Ni nani atakayeigeuza mioyo ya watoto iwaelekee mababa?

by Admin | 28 August 2019 08:46 pm08

Lakini ile sehemu ‘B’ ya maandiko ambayo inasema Eliya atakuja kabla haijaja ile siku ya KUOGOFYA , yaani ile siku ya kutisha ya Mungu Mwenyezi. hapa Eliya atakuja tena ili kuigeuza mioyo ya Watoto iwaelekee Baba zao.kumbuka Yohana mbatizaji alikuja kuigeuza Mioyo ya Baba iwaelekee wana, lakini sasa huyu atakuja kuigeuza mioyo ya Watoto iwaelekee Baba zao.

katika siku za mwisho ambazo ndizo tunazoishi sasa. Na watoto wanaozungumziwa hapo ni sisi tunaoishi sasa katika nyakati hizi za mwisho, na mababa ni Mitume wa Kristo wa kanisa la kwanza ambao mafundisho yao ni biblia ambayo ndio msingi wa Ukristo wa kweli.

hivyo basi Eliya huyu wa mwisho alioahidiwa ni kwa kazi moja tu ya kuturudisha sisi katika Ukristo wa biblia ambao kwa muda mwingi kama tunavyosoma katika historia ya ukristo uliingiliwa na mafundisho ya uongo nayo ni mafundisho ya mpinga Kristo ambayo kwenye ufunuo 2:6 “Kristo ameyakemea kama mafundisho ya wanikolai” ambayo leo hii tunaweza tukayaona ndani ya kanisa la Kristo.

hivyo basi Eliya wa kwanza (Yohana Mbatizaji) alitangulia kuja kwa kwanza kwa Kristo, na katika siku hizi za mwisho Mungu alimtuma ndugu WILLIAM MARRION BRANHAM kwa huduma kama ya Eliya  kwa kuliandaa kanisa kwa ajili ya kuja kwa pili kwa Kristo,na ujumbe Mkuu Bwana aliompa ni kuturudisha sisi kwenye Neno, yaani biblia na kulingana na Ufunuo 18:4.”…..tokeni kwake enyi watu wangu msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.”..huu ndio ujumbe wa bibi arusi safi wa  Kristo wa wakati huu wa mwisho.  Kutoka katika kamba za dini na Madhehebu na kurudi kuliishi Neno la Mungu. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

1.William Marrion Branham ni nani?

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/08/28/ni-nani-atakayeigeuza-mioyo-ya-watoto-iwaelekee-mababa/