Nilikuwa naomba kujua utofauti kati ya DHAMBI, UOVU na KOSA kibiblia.asante!!

by Admin | 31 August 2019 08:46 pm08

JIBU: DHAMBI: Kibiblia yale mambo yote yaliyokuwa yanafanyika kinyume na TORATI/SHERIA ya Mungu, yalikuwa yanajulikana kama DHAMBI. Ikiwa na maana kuwa mtu yeyote atakayeonekana ameivunja hiyo sheria ni sawa na amefanya dhambi au ameiasi sheria. Ilijulikana kuwa mtu huyo kabla ya kuiasi sheria yenyewe alijua kabisa jambo hilo analolifanya lilishahakikiwa na kutolewa rasmi kuwa ni makosa na kwamba mtu yeyote anayefanya hivyo hana udhuru, atastahili adhabu fulani, lakini yeye kwa makusudi anakwenda kufanya..Hiyo kwake inakuwa ni dhambi na haina huruma ni lazima atumize deni lake la kuadhibiwa. Kwamfano tunaona biblia ilikataza na hata sasa imekataza kuzini, au kuua, au kuabudu sanamu hivyo basi angali mtu akijua kabisa Mungu kakataza kufanya mambo hayo mapaka akaamua kuyaandika katika mawe, na nyingine katika kitabu halafu mtu huyo anaenda kuzini, au kuiba, au kuabudu sanamu kwa makusudi kabisa..Mtu huyo ndio tunasema kafanya dhambi/ kaiasi sheria.  

MAOVU: Kadhalika, na mambo mengine yote ambayo kwa namna moja au nyingine “hujayaonekana” au “hajaandikwa” katika Torati/Biblia lakini yanafanyika na inajulikana kabisa kwamba hayo mambo hayastahili kufanywa huku dhamira ya mtu mwenyewe ikimshuhudia ndani yake, na mtu akaenda kuyafanya hayo..Sasa hayo ndio yanajulikana kama MAOVU/MACHUKIZO. Mfano wa maovu tunaweza kuyaona yalitendeka katika kipindi cha Nuhu, na kipindi cha Sodoma na Gomora, kumbuka watu wa wakati ule walikuwa bado hawajapewa Torati/sheria kutoka kwa Mungu, kama tulionayo sisi. Tunasoma  

Mwanzo 6: 5 “Bwana akaona ya kuwa MAOVU ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote. 6 Bwana akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. 7 Bwana akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya. 8 Lakini Nuhu akapata neema machoni pa Bwana.”

Unaona hapo?. Kwahiyo mfano wa mambo yaliyokuwa yanatendeka kipindi kile mpaka yakapelekea dunia kuteketezwa ndiyo yaliyotabiriwa kutokea katika siku za mwisho kwamba maovu mengi yataongezeka.. Leo hii tunaweza kuona mambo mabaya hata yamezidi yale yaliyoandikwa kwenye biblia, yameijaza dunia, vitu kama uvutaji sigara, utoaji mimba, biashara haramu kama za watu, madawa ya kulevya,uchunaji ngozi, n.k. mambo ambayo hata kwenye biblia huwezi kuona yakitajwa moja kwa moja, lakini yanajulikana kuwa ni makosa, sasa haya yote ndiyo yanayoitwa MAOVU.  

KOSA: Na kosa, ni sawa na kutofanya kitu kisivyostahili. Kwa lugha rahisi mtu anaposema “Nimekosea” ni sawa na kusema amefanya kitu hicho isivyostahili. Mfano biblia inaposema.

Matendo 2:38 ” ….Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.”  

Halafu mtu anakwenda kumnyunyizia maji kichwani kama ishara ya ubatizo na kuepuka ubatizo wa maji ya kuzamishwa.kisha akatumie Jina lingine ambalo sio la YESU KRISTO kubatizia, sasa huyo mtu ni sawa na kafanya KOSA. Ametenda isivyostahili, (yaani kapindisha kile kilichoamriwa).   Hivyo ili mkristo uwe mtu asiwe na HILA, wala WAA, lolote mbele za Mungu, unapaswa uepuke yote matatu (yaani DHAMBI, MAOVU, MAKOSA)..Na haya yote unaweza ukayakwepa tu! endapo utafanya NENO LA MUNGU kuwa msingi pekee wa kuyaendesha maisha yako. Lakini kama utapenda kushikilia itikadi za dini fulani au dhehebu fulani, kumkosea Mungu, au kufanya dhambi au kutenda maovu huwezi kuepuka kwa namna yoyote ile.

DUMU katika maneno matakatifu ya Mungu, huku ukimwomba Mungu akufunulie njia sahihi ya kuiendea, na ukitia nia hiyo kwa kumaanisha, Roho Mtakatifu mwenyewe atakuongoza, na mwisho wa siku utajikuta unakuwa yule mwanawali mwerevu ambaye siku Bwana wake alipokuja alimkuta na mafuta ya ziada ndani yake(sasa yale mafuta ya ziada ni Ufunuo wa Roho mtakatifu), lakini wale wapumbavu hawakuwa na mafuta ya kutosha katika chupa zao, na pale Bwana wao alipokuja walikutwa hawana kitu, hivyo wakatupwa nje, ambapo kuna kuliko na vilio na kusaga meno. (Mathayo 25)  

Dunia ya leo imejaa maovu ya kila namna, usiruhusu uchukuliwe na namna ya dunia hii (Warumi 12:2). Hivyo ili mkristo uwe mtu asiwe na HILA, wala WAA, lolote mbele za Mungu, unapaswa uepuke yote matatu (yaani DHAMBI, MAOVU, MAKOSA)..Na haya yote unaweza ukayakwepa tu! endapo utafanya NENO LA MUNGU kuwa msingi pekee wa kuyaendesha maisha yako. Lakini kama utapenda kushikilia itikadi za dini fulani au dhehebu fulani, kumkosea Mungu, au kufanya dhambi au kutenda maovu huwezi kuepuka kwa namna yoyote ile.

Mungu akubariki. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/08/31/nilikuwa-naomba-kujua-utofauti-kati-ya-dhambi-uovu-na-kosa-kibiblia-asante/