Warumi 8:3″Maana yale yasiyowezekana kwa SHERIA,kwa vile ilivyokuwa DHAIFU kwa sababu ya MWILI”. Swali sheria ilikuwaje dhaifu kwasababu ya mwili?

Warumi 8:3″Maana yale yasiyowezekana kwa SHERIA,kwa vile ilivyokuwa DHAIFU kwa sababu ya MWILI”. Swali sheria ilikuwaje dhaifu kwasababu ya mwili?

JIBU: Sheria peke yake haiwezi kuondoa dhambi ndani ya mtu, kwamfano Mungu alipotoa amri usizini, Ni kweli wengi waliijitahidi kuishika kwa kutokuzini kabisa maisha yao yote mpaka kifo, lakini ukweli ni kwamba ile tamaa ya kutamani kuzini ilikuwepo ndani yao. Walijizuia vile ni kwasababu sheria ilisema hivyo, lakini sio kwamba ilitoka moyoni mwao kabisa kuchukia uasherati, Na ndio maana sheria hapo inaonekana kuwa dhaifu, kwasababu yenyewe kama yenyewe haiwezi kuondoa dhambi, bali ni kama inazuia tu kwa muda… wanaitumikisha miili kwa nguvu hata hivyo haisaidii kuondoa tamaa za mwili.

Lakini sheria ya Roho wa Mungu huondoa dhambi ndani ya moyo wa mtu kabisa, pale mtu anapozaliwa mara ya pili, ile kiu ya kutamani dhambi Mungu anaiua mwenyewe ndani ya mtu, hivyo mtu wa namna hiyo hata kama Mungu asingesema usizini, yeye mwenyewe kwa kuwa mafuta ya Roho wa Mungu yanakaa ndani yake, ataona kuwa kile kitendo ni kibaya, kadhalika kutamani nako ataona ni kubaya, kumchukia ndugu ni kubaya n.k….unaona hapo, utagundua kuwa zile sheria zote za Mungu zinatimilika zenyewe ndani ya moyo wa Mungu bila hata shuruti.

Warumi 8:1 Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.

2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.

Na ndio maana Bwana Yesu alisema, mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho hawezi kuuona ufalme wa mbinguni. Mtu hawezi kushinda dhambi kwa nguvu zake mwenyewe, nje ya Roho Mtakatifu. Wapo wanasema zishike amri kumi tu, basi inatosha kumpendeza Mungu…Lakini hawajui kuwa wapo wayahudi waliozikisha vizuri Zaidi ya wao lakini bado wakawa wanajiona kuwa hawana uzima ndani yao. Ni kwasababu gani?. Kwasababu sheria wanaishika kwa njia ya mwili lakini sio kwa njia ya Roho.

Ubarikiwe.


Mada zinazoendana:

UTIMILIFU WA TORATI.

MWISHO WA HAO WAMSAHAUO MUNGU.

UFALME WA MUNGU HAUPATIKANI KIRAHISI.

UKOMA NA UJANE ULIO NDANI YAKO, UMEUPATIA TIBA?

JINSI ITAKAVYOKUWA KATIKA SIKU ILE

FUVU LA KICHWA.

ALAMA KATIKA VIPAJI VYA NYUSO.

 

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Leave a Reply