Ashuru ni nchi gani kwa sasa?

by Admin | 11 March 2022 08:46 am03

Ashuru ni wapi?

Ashuru ilikuwa ni nchi iliyokuwepo maeneo ya Iraq, Uturuki, na Syria..Mataifa haya matatu yamechangia sehemu ya nchi hiyo ya Ashuru, kama vile mataifa matatu (Kenya, Uganda na Tanzania), yalivyo na sehemu katika ziwa Victoria, kadhalika na Iraq, Uturuki na Syria ni sehemu ya Taifa hilo liliokuwa linaitwa Ashuru.

Lakini kwasasa duniani hakuna Taifa linaloitwa Ashuru. Kwani baada ya mataifa hayo matatu kuzaliwa hilo la Ashuru likafa.

Na Uliokuwa mji mkuu wa Taifa la Ashuru, uliitwa NINAWI. Ninawi ndio mji Nabii Yona alioambiwa akahubiri Injili, lakini kinyume chake akakimbilia Tarshishi..Kujua Ninawi ni wapi kwa sasa fungua hapa>NINAWI.

Vile vile kujua Tarshihi ni wapi kwasasa fungua hapa > TARSHISHI.

Asili ya Taifa la Ashuru kibiblia ni kutoka kwa Nimrodi..

Mwanzo 10:8 “Kushi akamzaa Nimrodi, akaanza kuwa mtu hodari katika nchi.

9 Alikuwa hodari kuwinda wanyama mbele za Bwana. Kwa hiyo watu hunena, Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda wanyama mbele za Bwana.

10 Mwanzo wa ufalme wake ulikuwa Babeli na Ereku, na Akadi, na Kalne, katika nchi ya Shinari.

11 Akatoka katika nchi ile akaenda mpaka Ashuru, akajenga Ninawi, na Rehoboth-iri, na Kala;

12 na Reseni, kati ya Ninawi na Kala, nao ni mji mkubwa”.

Lakini Taifa la Ashuru ndilo lililowachukua Israeli na kuwapeleka utumwani katika Taifa hilo. Lakini baadaye walirudi katika Taifa lao chini ya amri ya Koreshi Mwajemi.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2022/03/11/ashuru-ni-nchi-gani-kwa-sasa/