SWALI: Mhubiri anamaana gani anaposema “Wala jambo jipya hakuna chini ya jua” na angali tukiangalia tunaona kila siku mambo mapya yanavumbiliwa mfano wa AI (artificial inteligence)? ambayo hayakuwepo zamani?.
JIBU: Kuelewa vizuri alimaanisha nini kwa kusema hivyo tuanzie vifungu vya juu kuitazama habari yote ililenga eneo lipi.
Mhubiri 1:2-11
[2]Mhubiri asema, Ubatili mtupu, ubatili mtupu, mambo yote ni ubatili. [3]Mtu ana faida gani ya kazi yake yote aifanyayo chini ya jua? [4]Kizazi huenda, kizazi huja; nayo dunia hudumu daima. [5]Jua lachomoza, na jua lashuka, na kufanya haraka kwenda mahali pa maawio yake. [6]Upepo huvuma kusi, hugeuka kuwa kaskazi; hugeuka daima katika mwendo wake, na upepo huyarudia mazunguko yake. [7]Mito yote huingia baharini, walakini bahari haijai; huko iendako mito, ndiko irudiko tena. [8]Mambo yote yamejaa uchovu usioneneka, jicho halishibi kuona, wala sikio halikinai kusikia. [9]Yaliyokuwako ndiyo yatakayokuwako; na yaliyotendeka ndiyo yatakayotendeka; wala jambo jipya hakuna chini ya jua. [10]Je! Kuna jambo lo lote ambalo watu husema juu yake, Tazama, ni jambo jipya? Limekwisha kuwako, tangu zamani za kale zilizokuwa kabla yetu sisi. [11]Hakuna kumbukumbu lo lote la vizazi vilivyotangulia; wala hakutakuwa na kumbukumbu lo lote la vizazi vitakavyokuja, miongoni mwao wale watakaofuata baadaye.
[2]Mhubiri asema, Ubatili mtupu, ubatili mtupu, mambo yote ni ubatili.
[3]Mtu ana faida gani ya kazi yake yote aifanyayo chini ya jua?
[4]Kizazi huenda, kizazi huja; nayo dunia hudumu daima.
[5]Jua lachomoza, na jua lashuka, na kufanya haraka kwenda mahali pa maawio yake.
[6]Upepo huvuma kusi, hugeuka kuwa kaskazi; hugeuka daima katika mwendo wake, na upepo huyarudia mazunguko yake.
[7]Mito yote huingia baharini, walakini bahari haijai; huko iendako mito, ndiko irudiko tena.
[8]Mambo yote yamejaa uchovu usioneneka, jicho halishibi kuona, wala sikio halikinai kusikia.
[9]Yaliyokuwako ndiyo yatakayokuwako; na yaliyotendeka ndiyo yatakayotendeka; wala jambo jipya hakuna chini ya jua.
[10]Je! Kuna jambo lo lote ambalo watu husema juu yake, Tazama, ni jambo jipya? Limekwisha kuwako, tangu zamani za kale zilizokuwa kabla yetu sisi.
[11]Hakuna kumbukumbu lo lote la vizazi vilivyotangulia; wala hakutakuwa na kumbukumbu lo lote la vizazi vitakavyokuja, miongoni mwao wale watakaofuata baadaye.
Ukichunguza hapo halengi uvumbuzi na maendeleo ya kibinadamu, kwasababu hata wakati wake Sulemani kulikuwa na mavumbuzi mengi tu yeye mwenyewe alisema;
Mhubiri 7:29
[29]Tazama, hili tu nimeliona; Mungu amemfanya mwanadamu mnyofu, lakini wamebuni mavumbuzi mengi.
Lakini alikuwa analenga ‘kazi ya Mungu aliyoifanya chini ya jua’ na ‘misingi ya mifumo ya kiulimwengu’ kwa ujumla, katika hayo hakuna jipya. ndio maana anasema jua huchomoza jua huzama, tangu zamani jua ni lile lie, ijapokuwa sayansi inakuwa, kamwe haliwezi siku moja nikachomoza la kijani, upepo ni ule ule unafuata mkondo wake, kamwe hauwezi tokea ardhini, kizazi kinakuja, kizazi kinakwenda hakuna jipya, mito ni ile ile inatiririka kamwe maji hayewezi kubadilika na kuongea, Yaani mwanadamu hata hajitahidi vipi, katika ujumla wake wa maisha atazunguka tu mulemule watu wa kale walipozunguka. Watu watazaliwa, watu watakufa.
Vilevile katika mifumo ya kiulimwengu, wafanyabiashara walikuwepo, watakuwepo, wajenzi walikwepo watakuwepo, maudhui ya maisha ni ile ile, ni mwonekano tu unabadilika, ni sawa na mtu aliyevaa leo suti, kesho kanzu, haviwezi kumbadili mtu na kumfanya malaika. Au unga wa ngano, leo utatengenezea chapati, kesho mkate, kesho kutwa maandazi, bado ngano ni ileile hakuna jipya ndani yake tukaona inazaa pilau.
Ndio maana maandiko yanatufundisha ni nini jambo sahihi la kufanya tuwapo duniani tusije kuta tunapoteza muda kudhani tunaweza leta jambo jipya duniani. Lakini tunafundishwa tumche Bwana, ndio jambo lenye maana linaloleta jambo jipya moyoni mwa mwanadamu, ambalo ni uzima wa milele.
Mhubiri anamalizia kwa kusema…
Mhubiri 12:13
[13]Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.
Je! Umeupokea wokovu wa Bwana Yesu? Kama ni La! Huu ndio wakati sahihi wa kupokea msamaha wa dhambi zako na uzima. Tubu ukabatizwe katika jina la Yesu Kristo, upokee ondoleo la dhambi zako na kipawa cha Roho Mtakatifu, atakayekusaidia kuishi maisha matakatifu. Ikiwa utapenda mwongozo huo basi fungua hapa kwa msaada huo.. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
MJUMBE WA AGANO.
NI KIZAZI KIPI WEWE UPO?(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)
SAUTI NYUMA YA ISHARA.(Opens in a new browser tab)
Rudi Nyumbani
Print this post