Je! Uvimbe unatibika?

by Admin | 31 July 2024 08:46 pm07

Jibu ni ndio.

Lakini sio njia zote zinaweza kutibu ugonjwa huo. Ni kweli madaktari hufanya kwa sehemu yao. Lakini Mungu hufanya zaidi, kwake yote hutibika.

Uvimbe wa aina yoyote ile, uwe ule wa kwenye mfuko wa uzazi, au kibofu, au  kwenye koo, au kichwa, au tumboni. Popote pale, maadamu ni uvimbe, haijalishi ukubwa wake, unaponyeka huo.

Na anayeweza kufanya hivyo ni YESU TU.

Tafsiri ya jina lake ni MWOKOZI. Ndiye aliyetumwa na Mungu mahususi kuwaokoa wanadamu na dhambi zao, pamoja na shida zao na magonjwa yao, alizaliwa kwa kusudi hilo tu moja. Hivyo maadamu yeye yupo huna haja ya kuwa na hofu.

Isaya 53:4 Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.  5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona

Huo ugonjwa alishauchukua zamani sana, kabla ya wewe kuzaliwa.  Alimponya Lazaro aliyekufa na ugonjwa, na kuzikwa na kuoza. Atakuponya na wewe, ambaye hata bado hujafa kwa ugonjwa huo. Ni kumwamini tu, basi,

Lakini hatua ya kwanza ni wewe kumpokea maishani mwako. Kukubali neema yake, kwa kutubu dhambi zako, kwa kumaanisha kabisa kuziacha, kisha yeye mwenyewe atakupa ondoleo la dhambi hizo, na utakuwa umeupokea uzima wa milele, Wala hatazikumbuka tena kuanzia siku hii ya leo na kuendelea.

Ikiwa upo tayari kupokea wokovu huu bure basi fungua hapa kwa mwongozo wa sala ya Toba >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Ikiwa sasa tayari umeokoka. Basi unahitaji msaada ya kimaombi.

Piga namba uzionazo chini ya chapisho hili nasi tutakuombea (bure) na kwa imani utapokea uponyaji wako.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

KANSA/SARATANI INATIBIKA.

SALA YA UPONYAJI/MAOMBI YA UPONYAJI.

UPONYAJI WA YESU.

JE! UKIMWI UNATIBIKA?

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/07/31/je-uvimbe-unatibika/