Kwanini tunaomba kwanza kabla ya kula chakula?
Kwasababu tumeagizwa na Bwana kwamba jambo lolote lile tulifanyalo, iwe kwa tendo au kwa Neno, tulifanye katika jina la Yesu Kristo. Ikiwa na maana tumtangulize Kristo, yeye awe ndio sababu ya mambo yote,
Wakolosai 3:17
[17]Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.
kwasababu katika hilo Kristo anatukuzwa ndani ya mambo yetu yote na si katika mambo baadhi tu.
1 Wakorintho 10:31
[31]Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.
Na ndio maana kabla hujahubiri unaomba, hujalala unaomba, hujaanza kikao unaomba, unapokwenda kazini unaomba, vilevile unapokula unapaswa uombe.
Je ni mambo gani ya kuzingatia katika sala yako ya chakula?
1) Kushukuru
2) Kutakasa
1 Timotheo 4:4-5
[4]Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani; [5]kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.
[4]Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani;
[5]kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.
Hivyo katika sala yako, hakikisha jambo la kwanza ni unamshukuru Mungu kwa kukupa rizki hiyo, ambayo unajua kabisa wapo watu wanakufa kila siku kwa kukosa kabisa hata hicho kidogo/kingi ulichokirimiwa.
Jambo la Pili, ni kukitakasa.. Hivyo unaomba Mungu akibariki kwa kukiponya, ili utakaposhiriki kikakutie nguvu na kukupa afya njema ili uweze kumtumikia Mungu vyema. Ukikumbuka kuwa vyakula tulavyo si vyote ni salama, vingine ni sumu, vingine vinauchafu , vingine vimenenewa maneno mabaya n.k. Hivyo ni kuhusisha utakaso kwa maombi.
Ukizingatia mambo hayo mawili katika maombi yako,(shukrani & utakaso) kama msingi, basi hata ukiongezea maneno mengine, utakuwa umeomba vema.
Huu ni mfano wa sala fupi ya kuombea chakula kabla hujashiriki.
“Bwana Yesu asante kwa rizki hii uliyoiweka mbele yangu, najua ni kwa neema yako nimepokea. Ninaomba uibariki na kuitakasa, hata ninapokwenda kuishiriki initie nguvu na afya njema nikakutumikie wewe vema. Ni maombi yangu, pia uwajalie na wale ambao hawajapata rizki yao popote pale walipo. Ninaomba haya nikiamini ni katika jina la Yesu Kristo. Amen”
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
MISTARI YA KUOMBEA AMANI YA FAMILIA.
MAOMBI YA KUOMBEA WATOTO.
MWONGOZO WA MAOMBI YA ASUBUHI.
Rudi Nyumbani
Print this post