Nini maana ya “mtu asimpunje ndugu yake” (1Wathesalonike 4:6 ).

by Admin | 25 November 2024 08:46 pm11

Swali: Kupunja kibiblia ni kufanya nini?…au maana yake nini mstari huo wa 1Wathesalonike 4:6 ?


Jibu: Turejee..

1Wathesalonike 4:6  “Mtu asimpunje ndugu yake wala kumkosa katika jambo hili; kwa sababu Bwana ndiye alipizaye kisasi cha haya yote; kama tulivyowaambia kwanza, tukashuhudia sana”.

Kupunja kunakozungumziwa ni “kudhulumu”… Na dhulumu inayozungumziwa hapo si ile ya kupunjwa kiwango cha nafaka sokoni bali ni ile ya Ndoa.

Hivyo kiswahili chepesi cha mstari huo ni hiki… “Mtu asimdhulumu ndugu yake wala kumkosa katika jambo hili (Mke/Mume); kwa sababu Bwana ndiye alipizaye kisasi cha haya yote; kama tulivyowaambia kwanza, tukashuhudia sana ”

Na tunajuaje dhulumu inayotajwa hapo ni ile ya Mke au Mume?

Tukianzia juu kidogo katika ule mstari wa tatu, tunaona Mtume Paulo kwa uongozo wa Roho analionya kanisa juu ya  Uasherati, kwamba kila mmoja ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na si katika tamaa za uasherati kama watu wa wasiomjua Mungu.

1Wathesalonike 4:3  “Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati;

4  kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima;

5  si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu.

6  Mtu asimpunje ndugu yake wala kumkosa katika jambo hili; kwa sababu Bwana ndiye alipizaye kisasi cha haya yote; kama tulivyowaambia kwanza, tukashuhudia sana”.

Hivyo Unapomchukua Mke au Mume wa ndugu yako, fahamu kuwa unafanya jambo baya sana na lenye kumchukiza Mungu. Na tena maandiko yanasema kuwa Bwana ndiye alipizaye kisasi.. Maana yake ukimchukua mke/mume wa ndugu yangu, Bwana atakulipa kisasi hapa hapa duniani, na kama hautatubu na kumwacha huyo mke/mume basi pia hukumu ya ziwa la moto hutaiepuka.

Vile vile kama unamsaliti Mke/Mume wako na kwenda kuoa/kuolewa na mwingine, kisasi cha Bwana kipo juu yako, maumivu utakayomwachia mwingine utayalipa hapa hapa duniani na kama usipotubu pia adhabu ya ziwa la moto, utaenda kukutana nayo, na hiyo si hukumu ya wanadamu bali ya MUNGU.

Biblia inasema Ndoa na iheshimiwe na watu wote (Waebrania 13:4).. Anaposema “wote” maana yake hata wasio wahusika wa hiyo ndoa, wameamriwa waiheshimu ndoa ya watu hao. Hivyo ukiharibu ndoa ya wengine kwasababu yoyote ile, Bwana atakulipa kisasi, hiyo ni biblia!.

Maran atha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

KISASI NI JUU YA BWANA.

NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE.

Ipi tofauti ya Ulawiti na Ufiraji (1Wakorintho 6:9)?

MAANA ROHO HUCHUNGUZA YOTE, HATA MAFUMBO YA MUNGU.

Je YUDA alikuwa ni shetani kulingana na Yohana 6:70?

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/11/25/nini-maana-ya-mtu-asimpunje-ndugu-yake-1wathesalonike-46/