by Admin | 25 November 2024 08:46 pm11
Jibu: Turejee.
Zaburi 119:70 “Mioyo yao imenenepa kama SHAHAMU, Mimi nimeifurahia sheria yako”.
“Shahamu” ni mafuta yaliyo katika nyama… Karibia viumbe vyote vyenye damu na nyama, vinayo shahamu, mwanadamu au mnyama mwenye shahamu nyingi anaonekana amenona, na kinyume chake mwenye kiwango kidogo cha shahamu, anaeonekana kakonda.
Andiko lingine linalotaja shahamu ni pamoja na Kumbukumbu 32:38 na Isaya 34:7..
Isaya 34:7 “Na nyati watatelemka pamoja nao, na mahasai pamoja na mafahali, na nchi yao italewa kwa damu, na mavumbi yake yatanoneshwa kwa shahamu.
8 Maana ni siku ya kisasi cha Bwana, mwaka wa malipo, ili kushindania Sayuni”
Lakini tukirejea katika hiyo Zaburi 119:70 inasema “Mioyo yao imenenepa kama SHAHAMU, Mimi nimeifurahia sheria yako”.
Hapo biblia inatufundisha ni kipi cha kujinenepesha nacho Zaidi… kwamba SHERIA ZA MUNGU, ndio kitu tujinenepeshe nacho Zaidi kuliko SHAHAMU.
Sasa si vibaya kula vyakula vya shahamu, na kunenepa kwa shahamu (mafuta)… lakini kama tutanenepa kwa shahamu halafu hatujanepa katika sheria za MUNGU basi unono wetu ni bure. Lakini ni heri kunenepa kwa sheria za Mungu, na Neno lake, kwasababu roho ni bora kuliko mwili.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
MANENO YA MUNGU YANAPINDULIWAJE?
JE! UMEYABATILISHA MAMBO YA KITOTO?
Kuna tofauti gani kati ya “Edeni” na “Adeni”?
NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?
KWANINI DAUDI ALIKUWA NI MTU ALIYEUPENDEZA MOYO WA MUNGU?
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/11/25/shahamu-ni-nini-zaburi-11970/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.