SWALI: Wanawake wenye cheo wanaotajwa kwenye biblia ni akina nani? (Matendo 17:12)
JIBU: Mitume walipoanza kulitekeleza agizo kuu la Bwana Yesu la kuenenda ulimwenguni kote kuhubiri injili, biblia inatuonyesha walikutana na makundi mbalimbali ya walioamini.
Sasa mojawapo ya kundi hilo ambalo liliipokea injili, walikuwa ni hawa wanawake wenye cheo.
Kwamfano tunaweza kuona jambo hilo katika ziara ya mtume Paulo kule Beroya.. alipofika kule alikutana wa wanawake wa namna hii, na akawahubiria wakaipokea injili.
Matendo ya Mitume 17:10-12
[10]Mara hao ndugu wakawapeleka Paulo na Sila usiku hata Beroya. Nao walipofika huko wakaingia katika sinagogi la Wayahudi. [11]Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo. [12]Basi watu wengi miongoni mwao wakaamini, na wanawake wa Kiyunani wenye cheo, na wanaume si wachache.
[10]Mara hao ndugu wakawapeleka Paulo na Sila usiku hata Beroya. Nao walipofika huko wakaingia katika sinagogi la Wayahudi.
[11]Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.
[12]Basi watu wengi miongoni mwao wakaamini, na wanawake wa Kiyunani wenye cheo, na wanaume si wachache.
Wanawake wenye cheo ni wanawake waliokuwa na sifa ya aidha nafasi za juu za kiutalawa, au ushawishi mkubwa kwenye jamii zao au wenye mali nyingi.
Wengi wao walipokutana na injili ya kweli ya Bwana Yesu Kristo waliipokea na kugeuka.
Lakini tunaona mahali pengine, mtume Paulo alipokwenda, wayahudi walimfanyia fitina kwa kuwatumia watu wa namna hii ili kuwataabisha..Kwamfano alipofika kule Antiokia mji wa Pisidia, na kuhubiri injili kwa ushujaa na wengi kuokoka. Wayahudi kwa sababu ya wivu wakawashawishi baadhi ya wanawake na wanaume wa namna hii..Ili wawapinge akina Paulo. Kwasababu walijua nguvu yao kijamii ni kubwa kiasi gani, hivyo itakuwa rahisi kutekeleza adhma yao.
Matendo ya Mitume 13:50
[50]Lakini Wayahudi wakawafitinisha wanawake watauwa wenye cheo na wakuu wa mji, wakawataharakisha watu wawaudhi Paulo na Barnaba; wakawatoa katika mipaka yao.
Hivyo hiyo ni kututhibitishia hata sasa, Watu wenye vyeo wana nafasi ya kuwa washirika wa injili. Hivyo tusibague wa kumuhubiria, kwasababu wote Kristo amewafia msalabani. awe ni mbunge, au waziri, awe ni tajiri, au maskini, msomi, au asiye na elimu,. wote ni wa Mungu na wanastahili wokovu, wasipotumiwa na Mungu wao, shetani atawatumia. Hivyo nguvu zetu za injili ziwe sawasawa kwa watu wote.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Mabibi wastahiki walikuwa ni watu gani? (Esta 1:18).
Apitaye cheo ni mtu wa namna gani?
Wale waliowekewa tayari ufalme ni akina nani?. (Mathayo 20:23).
Rudi Nyumbani
Print this post