Lango la samaki lilikuwaje? (Sefania 1:10)

by Admin | 27 November 2024 08:46 am11

.Swali: Hili lango la samaki linalotajwa katika Sefania 1:10 lilikuwaje na lilikuwa linahusika na nini?.


Jibu: Yalikuwepo malango kadhaa ya Kulikuwa mji wa Yerusalemu nyakati za zamani, ambayo yalizunguka pande zote za mji.

Baadhi ya  malango hayo ni Lango la “Lango la kale”, “Lango jipya” “Lango la Efraimu” na “Lango la kondoo”, ambalo liitumika kupitishia kondoo katika mji, kwa maelezo marefu juu ya lango hilo fungua hapa >>>

Mlango la kondoo ulikuwaje?(Yohana 5:2)

Lakini kuhusu “Lango la Samaki” turejee maandiko.

Sefania 1:10 “Na katika siku ile, asema BWANA kutakuwako sauti ya kilio kutoka lango la samaki, na mlio mkuu katika mtaa wa pili, na mshindo mkuu kutoka milimani”.

Hili “Lango la Samaki” halikuwa na matumizi kama lile “Lango la Kondoo”…kwamba linatumika kupitisha samaki ndani ya mji.

La! Bali ni lango la mji wa Yerusalemu ambalo lilikuwa upande Kaskazini-magaribi, karibu  na “Soko la Samaki”..Hivyo liliitwa jina hilo kufuatia soko la samaki lililokuwa karibu na lango hilo.

Ingawa pia kwasababu lilikuwa upande wa kaskazini, wafanya biashara kutoka Galilaya walilitumia hili, na wengi waliotoka Galilaya walikuwa ni Wavuvi..

Hivyo lilitumika pia na wafanya biashara wa samaki, lakini halikuitwa kwasababu hiyo bali kutokana na soko hilo la samaki lilikokuwa karibu na lango hilo.

Lango la samaki kwanza limeanza kuonekana kipindi cha Mfalme Manase ambaye alikuja kuujenga ukuta wa nje wa mji wa Daudi (Yerusalemu), aliujenga upande wa magharibi mpaka kufikia mlango huo wa samaki.

2 Nyakati 33:12-14

“Hata alipokuwa katika taabu, akamsihi BWANA, Mungu wake, akajinyenyekeza sana mbele za Mungu wa baba zake.

13 Akamwomba; naye akamtakabali, akayasikia maombi yake; akamrudisha tena Yerusalemu katika ufalme wake. Ndipo Manase akajua ya kwamba BWANA ndiye Mungu.

14 Hata baada ya hayo akaujengea mji wa Daudi ukuta wa nje, upande wa magharibi wa Gihoni, bondeni, hata kufika maingilio ya LANGO LA SAMAKI; akauzungusha Ofeli, akauinua juu sana; akaweka maakida mashujaa katika miji yote ya Yuda yenye maboma”.

Baada ya miaka mingi kupita, tunakuja kusoma, kipindi ambacho mji wa Yerusalemu umebomolewa na Nehemia amerudi kuujenga ukuta, tunaona biblia inataja kuwa sehemu ya ukuta ya upande wa “Lango la samaki” ulijengwa na wana wa Senaa..

Nehemia 3:3 “Na lango la samaki wakalijenga wana wa Senaa; wakazitia boriti zake, wakaisimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake”.

Utaona tena lango hilo linatajwa kipindi cha mji kuwekwa wakfu (Nehemia 12:39).

Je umempokea Bwana YESU?..Je unafahamu kuwa tunaishi katika majira ya kurudi kwa YESU kwa pili?.

Je akija leo na kukukuta hivyo ulivyo utakwenda naye??

Bwana atusaidie sote.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/11/27/lango-la-samaki-lilikuwaje-sefania-110/