by Admin | 28 November 2024 08:46 pm11
SWALI: Biblia inamaana gani kusema..maana Mungu wetu ni moto ulao?
Waebrania 12:29
[29]maana Mungu wetu ni moto ulao.
JIBU: Andiko hilo linaeleza sifa nyingine ya Mungu, kwamba si tu anajifananisha na maji, au nuru, au mafuta bali pia na “moto” tena ule “moto ulao”.
Kwanini aseme hivyo?
Ukianzia kusoma mistari ya juu utaona anaeleza madhara ya kuikataa sauti ya Kristo, kwamba ghadhabu yake inapokuja huwa ni mbaya mfano tu wa ile ghadhabu aliyoidhihirisha kwa wana wa Israeli kule jangwani walipoasi.
Waebrania 12:25
[25]Angalieni msimkatae yeye anenaye. Maana ikiwa hawakuokoka wale waliomkataa yeye aliyewaonya juu ya nchi, zaidi sana hatutaokoka sisi tukijiepusha na yeye atuonyaye kutoka mbinguni;
Neno hili la moto ulao, mwandishi alilinukuu kwenye vifungu hivi vya agano la kale.
Kumbukumbu la Torati 4:23-24
[23]Jihadharini nafsi zenu, msije mkalisahau agano la BWANA, Mungu wenu, alilolifanya nanyi, mkajifanyia sanamu ya kuchonga, mfano wa umbo la kitu cho chote ulichokatazwa na BWANA, Mungu wenu,
[24]kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, ni moto ulao, Mungu mwenye wivu.
Mungu alijitambulisha kwa wana wa Israeli kwa sifa hii, ndio sababu hata mwanzoni kabisa alipomtokea Musa kule jangwani alijifunua kama kijiti kinachoungua lakini hakiteketei. Kufunua kuwa wakitembea katika njia zake moto wake hauwezi kuwala, hivyo wasiwe na hofu, bali utawalinda na kuwaimarisha,lakini wakiasi utawala hakika.
Moto huo ndio ule uliokuwa nguzo mbele yao kuwalinda. Na walipokosea waliadhibiwa kwa huo, wakaanguka watu wengi jangwani kwa yale mapigo tunayoyasoma.
Sasa tukirudi kwenye kitabu cha Waebrania. mwandishi anatoa angalizo pia kwamba tusiipuuzie sauti ya Mungu katika Kristo Yesu, kwasababu sasa hivi Mungu anazungumza na sisi moja kwa moja kutoka mbinguni, sio tena kwenye mahema au milimani,kama kule jangwani, hivyo tuongeze umakini
Tukikumbuka kuwa sifa zake ni zile zile…Yeye ni moto ulao hata sasa. Tunapofanya dhambi kwa makusudi tunapokengeuka na kudharau wokovu (Waebrania 6:4-8)…tuogope kwasababu moto wa wivu wake unaweza pita juu yetu, na kutuharibu kabisa, na kujikuta tupo katika ziwa la moto.
Lakini tunapotii, moto wake hautuharibu bali unatulinda na kutuimarisha..tunafananishwa na dhahabu, inayopitishwa kwenye moto kutakaswa.
Hivyo, maaana ya vifungu hivyo ni tunafahishwa kuwa Mungu ana sifa ya moto, tukilifahamu hilo tutautumiza wokovu wetu kwa kuogopa na kutetemeka. (Wafilipi 2:12). Wala hatutakwenda kutenda dhambi kwa makusudi.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>
https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Biblia inamaana gani inaposema ‘tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao’?
Rudi Nyumbani
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/11/28/maana-mungu-wetu-ni-moto-ulao-waebrania-1229/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.