Nini maana ya dhabihu na matoleo hukutaka? (Waebrania 10:5).

by Admin | 13 December 2024 08:46 am12

Swali: Je Mungu hapendezwi na dhabihu na matoleo, kulingana na mstari huo?


Jibu: Turejee..

Waebrania 10:5 “Kwa hiyo ajapo ulimwenguni, asema,

Dhabihu na toleo hukutaka, Lakini mwili uliniwekea tayari”.

Andiko hili limerejewa kutoka katika Zaburi 40:6, tusome ili tupate maana kamili.

Zaburi 40:6 “Dhabihu na matoleo hukupendezwa nazo,

Masikio yangu umeyazibua, Kafara na sadaka za dhambi hukuzitaka”.

Hapo imewekwa vizuri kuwa ni kafara na sadaka zinazotolewa kwaajili ya DHAMBI!! ndizo asizozitaka…

Sasa Dhabihu ni sadaka za kuteketezwa (ambazo ni kafara za wanyama) zilizokuwa zinatolewa kipindi cha agano la kale kwaajili ya kufunika dhambi..

Na kasoro ya dhabihu za wanyama ndio hiyo, ilikuwa haiondoi dhambi bali inafunika tu..

Kwahiyo hapo anaposema “Dhabihu na matoleo hukutaka”.. alimaanisha kuwa hizo dhabihu za wanyama hazifai katika kumwondolea mtu makosa yake na kumtakasa bali mwili wa Yesu na damu yake ndio iwezayo kumtakasa mtu na kumwondolea kabisa dhambi zake.

Ndivyo maandiko yasemavyo kuwa damu za mbuzi na mafahali haziwezi kuondoa dhambi na kumtakasa mtu bali zilikuwa zinafunika tu.

Waebrania 10:3 “Lakini katika dhabihu hizo liko kumbukumbu la dhambi kila mwaka.

4 Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi”

Lakini dhabihu ya mwili wa YESU, kupitia kumwagika kwa damu yake, unaondoa kabisa dhambi… Na hiyo ndio sadaka Mungu aliyoihitaji na sio dhabihu za kondoo na mbuzi na mafahali.

Waebrania 10:10 “Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu”.

Lakini kuhusiana na utoaji wa sadaka ni kwaajili ya shukrani, au kwaajili ya kazi ya ufalme wa mbinguni ni jambo linalompendeza Mungu na lenye baraka.

Lakini kama ni kwaajili ya dhambi (hakuna sadaka inayoweza kuondoa dhambi)..isipokuwa damu ya YESU ambayo tayari tumeshalipiwa bureee… tunachopaswa kufanya ili sadaka hiyo ifanye kazi juu yetu ni KUTUBU TU kwa kumaanisha kabisa kuacha dhambi!.

Tukiweza kutubu kwa kumaanisha basi tunapata msamaha na ondoleo la dhambi bure.

Je unaye YESU maishani?.

Kumbuka daima kuwa mwisho wa dunia upo, kama tu vile mwisho wa maisha ulivyo, ikiwa leo hii damu ya YESU si kitu cha thamani kwako, utasimamaje siku ile ya mwisho mbele zake?..Tafakari mara mbili.

Maran atha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/12/13/nini-maana-ya-dhabihu-na-matoleo-hukutaka-waebrania-105/