Jibu: Hakuna maelezo ya moja kwa moja katika biblia yanayoonyesha kuwa kula nyama mbichi ni dhambi,
Lakini vipo vielelezo vichache katika maandiko vinavyoonyesha kuwa si vizuri/si sahihi kula nyama mbichi.
Wakati wana wa Israeli wanatolewa Misri, ule usiku Bwana MUNGU aliwaambia waile pasaka, ambapo waliagizwa wamtwae mwanakondoo na kumooka motoni, wamle pamoja na mboga chungu lakini wasimle mbichi.
Kutoka 12:8 “Watakula nyama yake usiku ule ule, imeokwa motoni, pamoja na mkate usiotiwa chachu; tena pamoja na mboga zenye uchungu.
9 MSIILE MBICHI, wala ya kutokoswa majini, bali imeokwa motoni; kichwa chake pamoja na miguu yake, na nyama zake za ndani”.
Kwa asili Ulaji wa nyama mbichi ni hatari kwa afya ya mwili, kwani nyama mbichi ina minyoo na wadudu wengi wasiionekana kwa macho ambao ni hatari kwa afya na tumepewa maagizo ya kuitunza hii miili..lakini nyama iliyopikwa inakuwa salama kwani inaea vimelea hivyo…
Na pia ulaji wa nyama mbichi unaweza kuashiria uwepo wa roho nyingine ndani ya mtu, na mara nyingi roho ya ukatili inawaingia watu walao nyama mbichi (kwani wanyama ndio walao nyama mbichi).
Na pia ulaji wa nyama mbichi unahusiana na imani za kishirikina na imani nyingine potofu…
Hivyo si vyema kula nyama mbichi kama wanyama.
Bwana akubariki.