Jibu: Turejee…
Mwanzo 24:59 “Ndipo wakampeleka Rebeka ndugu yao, na YAYA wake, na mtumishi wa Ibrahimu, na watu wake”.
Yaya maana yake ni muuguzi (yaani mwangalizi wa mtu aliye katika udhaifu fulani au ugonjwa)...kwa kiswahili kingine chepesi ni NESI.
Kwahiyo Rebeka wakati anachukuliwa ili apelekwa kwa Isaka…aliambatana na Nesi wake huyo(Yaya).
Sasa biblia haijaelezea kwa undani sababu za kwenda naye, kwamba ni kwasababu za ugonjwa Rebeka aliokuwa nao (ambao pia haujatajwa) au labda kwa dharura endapo angepata shida fulani katika njia anayoiendea basi apate msaidizi kwani safari ile ilikuwa ni ndefu sana….
Au labda alimuhitaji yaya mbeleni katika maisha yake ya ndoa, baada ya kujifungua n.k hakuna anayejua, biblia imesema tu alienda na Yaya wake.
Neno hili pia limeonekana sehemu nyingine katika biblia..
2 Samweli 4:4 “Naye Yonathani, mwana wa Sauli alikuwa na mwana aliyekuwa na kilema cha miguu. Alikuwa amepata miaka mitano, habari za Sauli na Yonathani zilipofika Yezreeli, na yaya wake akamchukua akakimbia ikawa, alipokimbia kwa haraka, huyo mtoto akaanguka, akawa kilema. Na jina lake aliitwa Mefiboshethi”
Soma pia 2Nyakati 22:11 utaona pia neno hilo.
Naam kiroho YAYA wetu ni YESU KRISTO, tuwapo wadhaifu au katika dhiki au hali za kuishiwa nguvu na kuhitaji msaada, ni YESU KRISTO tu pekee awezaye kututunza na kututoa katika hizo hali.
Lakini Bwana hawezi kuwa mlezi wetu ikiwa hatutamruhusu awe hivyo, lakini tukiruhusu aingie maishani mwetu, na pia tukimheshimu na kuzishika amri zake hakika hatatuacha katika mateso sawasawa na ahadi zake.
Zaburi 41:3 “BWANA atamtegemeza alipo mgonjwa kitandani. Katika ugonjwa wake umemtandikia”
Je unaye YESU moyoni, na je maisha yako yanaakisi wokovu wa kweli?.
Kama bado upo nje ya YESU tafuta msaada mapema kwa YESU kabla mambo hayajaharibika zaidi.