Katika sheria za Mahakama inapotokea mfungwa aliyehukumiwa kifungo, akafariki katikati ya kifungo hiko, na ikathibitishwa na jeshi la magereza pamoja na ripoti za madaktari, na akazikwa basi kile kifungo chake kinakuwa kimefika mwisho, na kesi yake inakuwa haiendelei tena (inafutwa)..
Sasa ikitokea yule mtu akafufuka baada ya siku kadhaa anakuwa hana kesi tena (yupo huru) kwani kesi yake ilishafutwa, kutokana na ripoti za mahakama na madaktari..
Na zaidi sana mahakama haziamini ufufuo, hivyo itaendelea kuamini kuwa yule mtu alishakufa na taarifa zilithibtishwa na jeshi la magereza pamoja na madaktari.
Sasa ni hivyo hivyo kwa Bwana YESU, yeye alikubali kubeba hatia zetu na makosa yetu yaliyo mengi na akakubali kuhukumiwa kama yeye ndiye aliyeyatenda yale makosa..
Lakini alipokuwa anaanza kukitumikia kile kifungo kwa mateso makali (ambayo kiuhalisia yamgekuwa ya daima)..alikufa katikati..
Na sheria ya hukumu ni kwamba kifo kinahitimisha kifungo cha Mtu, hivyo Kristo alipokufa kifungo chake cha adhabu na mateso kikafikia mwisho, akawa hana hatia tena wala ule mzigo wa dhambi (yupo huru na dhambi sawasawa na maandiko).
Warumi 6:7 “kwa kuwa yeye aliyekufa amehesabiwa haki mbali na dhambi”
Lakini muujiza ni kwamba baada ya siku tatu akaonekana yu hai, na kwasababu hukumu yake ilishafutwa kwa kifo chake, akawa huru na kifungo hiko baada ya kufufuka, ndio maana hatuoni akilia kwa uchungu wa maumivu baadaa kufufuka, bali tunaona ana utukufu mwingi.
Kwahiyo laiti Kristo asingekufa angeendelea kuhesabika laana na mwenye hatia kwaajili ya dhambi zetu nyingi alizozobeba, ingempasa aendelee kukaa katika hali ya adhabu daima, na aendelee kutengwa na MUNGU daima.
Wagalatia 3:13 “Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti”
Lakini kifo chake kimehitimisha hukumu yake, ambayo sisi ndio tungepaswa tuitumikie.
Sasa tunapomwamini ndipo tunaingia katika huo mkondo wa kuondolewa dhambi..
Lakini tunapomkataa basi dhambi zetu zinabaki palepale..ni rahisi tu hivyo!.
Je umemwamini Bwana YESU?..Je umebatizwa kwa ubatizo sahihi wa Maji mengi na wa Roho Mtakatifu?.
Kama bado unasubiri nini?…je bado huoni tu gharama kubwa Bwana YESU aliyoingia kwaajili yetu ili tupate ondoleo la dhambi?.
Mpokee YESU leo wala usingoje kesho.
Maran atha!