by Admin | 21 April 2025 08:46 pm04
Swali: Bwana YESU aliposema kuwa “wala hakuna mmoja wenu aniulizaye unakwenda wapi” alimaanisha nini? (Yohana 16:5)?
Jibu: Turejee..
Yohana 16:5 “Lakini sasa mimi naenda zangu kwake yeye aliyenipeleka, WALA HAKUNA MMOJA WENU ANIULIZAYE, UNAKWENDAPI?
6 Ila kwa sababu nimewaambia hayo HUZUNI IMEJAA MIOYONI MWENU”.
Maneno haya Bwana YESU aliwaambia wanafunzi wake usiku ule mmoja kabla ya kusulibiwa kwake kwamba umefika wakati wa yeye kuondoka na kuwaacha….Na kwasababu ni maneno ya kuhuzunisha, wanafunzi wake waliingiwa na hisia kiasi cha kushindwa hata kumwuliza anakokwenda.
Si kwamba walikuwa hawataki kujua Bwana anakokwenda, La! Walikuwa wanatamani sana…lakini ile hali tu ya kufikiri kumwuliza hivyo haikuwa katika vichwa vyao kwa wakati ule, kwani walikuwa wanatafakari zaidi ni nini kitaendelea kwao baada ya Bwana kuondoka!.. Hivyo hiyo ikazuia hata kufikiri kumwuliza anakokwenda!.
Naam hata taarifa za mtu kufariki zinapowafikia wafiwa, ni wafiwa wachache sana wanaweza kufikiri Yule mtu ameenda wapi, wengi wanaishia kuhuzunika na kufikiri maisha ya upweke watakayokumbana nayo baada ya hapo kwa kumkosa Yule mtu katika kipindi chote cha maisha yao!.
Ndivyo ilivyokuwa kwa wanafunzi wa YESU, hisia zilifunika tafakari ndani yao, na Kristo aliliona hilo, ndipo akawaambia yale maneno kwamba yafaa yeye aondoke ili msaidizi aje (yaani Roho Mtakatifu), nao watapokea nguvu mpya.
Yohana 16:6 “Ila kwa sababu nimewaambia hayo huzuni imejaa mioyoni mwenu.
7 Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu”.
Na wakati ulipofika wa Roho Mtakatifu kushuka juu yao, wote walipokea nguvu kana kwamba BWANA YESU mwenyewe katika mwili anatembea nao, huzuni na unyonge wote ulipotea na badala yake ujasiri na nguvu viliingia ndani yao.
Je na wewe umempokea Roho Mtakatifu?.. kama bado basi mwamini Bwana YESU, na tubu dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha kisha tafuta ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Bwana YESU KRISTO sawasawa na Matendo 2:38, na Bwana atakupa kipawa hiko.
Matendo 2:38 “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie”.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
VIASHIRIA VINGINE VYA ROHO MTAKATIFU KUWEPO NDANI YAKO.
KUWA NA MAFUTA YOTE YA ROHO MTAKATIFU NDANI YAKO.
ZIFAHAMU KARAMA 9 ZA ROHO MTAKATIFU NA UTENDAJI KAZI WAKE.
ZIFAHAMU KAZI TATU ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA ULIMWENGU.
Nitaitofautishaje sauti ya Malaika na ya Roho Mtakatifu?
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/04/21/hakuna-aniulizaye-unakwenda-wapi-maana-yake-nini-yohana-165/
Copyright ©2025 unless otherwise noted.