by Devis | 9 May 2025 08:46 am05
JIBU: Haya ni maneno ya kiyunani, yanayoeleza namna tofauti ya kutafsiri maandishi.
Ni namna ya kutafsiri maandiko kwa kuzingatia mtazamo wa awali uliokusudiwa na mwandishi, kwa kuzingatia muktadha, hali ya kihistoria, matamshi na matumizi ya lugha.
Ni namna ya kutafsiri Maandiko kwa namna ya mtazamo wa mtu mwenyewe, kwa kulileta andiko liendane Na wazo lake binafsi,. Namna hii haitilii maanani sana kusudio La kwanza la mwandishi, bali lile aliaminilio kuwa ni sahihi Kwake. (Mfano wa hii ni ile namna ya kusema nimefunuliwa)
Kwa ufupi eksejesisi ni Kuliruhusu andiko lijitafsiri lenyewe huku Eisojesisi ni lilete andiko litafsiri ninachokitaka au kiamini.
Ijapokuwa Eksejesisi,(tafsiri ya awali) ndio msingi hasaa wa kusimamia katika kuyaelewa maandiko lakini eisojesisi pia Mungu huitumia kusema na sisi katika nyakati Fulani.
La kuzingatia ni kwamba kabla hujaipokea namna nyingine.. Ifahamu kwanza asili ya kwanza ya andiko hilo, ilikuwa ni nini.
Kwamfano Bwana Yesu aliposema.
Mathayo 11:28
[28]Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
Katika Eksejesisi hiyo mizigo inayozungumziwa hapo na Bwana Yesu sio umaskini, Mateso, madeni, familia, majukumu,n.k. hapana, bali mizigo ya dhambi. Ndicho Bwana Yesu alichomaanisha na kusudi la kwanza lililomfanya kuja duniani lilikuwa ni hilo kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi zake.
Lakini pia Bwana anaweza tumia andiko hilo kulenga na mizigo mingine, kwasababu ni ukweli usiopingika alisema pia tumtwike yeye fadhaa zetu zote.
1 Petro 5:7
[7]huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.
Hivyo namna zote Mungu anaweza kutumia kutujenga. Kwasababu Neno lake ni pana na njia zake hazichunguziki, katika kuwajenga, kuwafariji na kuwaponya watu. Isipokuwa hatari inakuja mtu kukosa kulipambanua vizuri Neno na matokeo yake kutegemea zaidi mtazamo (alioupokea), na kuacha biblia yenyewe kujieleza.
Hii ndio Imekuwa chumbuko la mafundisho mengi ya uongo, na potofu, kwamfano mtu atasema chapa ya mnyama (ufunuo 13) Ni ugonjwa wa Korona (covid-19). Wakati si kweli.
Au mtu atasema Yesu alitengeneza matope kwa mate yake akampaka mtu machoni akaona,(Yohana 9:6-7) hivyo na sisi kufanya kwa namna hiyo si kosa. Kumbe lile lilikuwa ni “ingilio la Mungu” la wakati husika lakini sio agizo la kudumu. Kwani agizo la daima ni kutumia jina la Yesu kutenda/kuamuru jambo lolote.(Kol 3:17)
Hivyo ili kubaki katika upande sahihi ni vema ukajifunza eksejesisi, (kufahamu muktadha wa kimaandiko), na ndio pale esiojesisi inapokuja Basi unaeweza Kuligawanya vema Neno la Mungu. Bila kuleta uharibifu/ madhara yoyote, katika imani au kwa kile unachowafundisha wengine.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/05/09/kati-ya-exegesis-na-eisegesis-ni-ipi-namna-bora-ya-kutafsiri-maandiko/
Copyright ©2025 Wingu la Mashahidi unless otherwise noted.