by Devis | 21 July 2025 08:46 am07
Mfalme mmoja wa Israeli aliyeitwa Yoashiliingiwa na wazo la kutaka kuikarabati nyumba ya Mungu (Hekalu), na kuamsha tena shughuli za kiibada zilizokuwa zimeharibiwa Na watawala wabovu waliotangulia..
Hivyo kwa kuwa alijua ukarabati unahitaji fedha, alichukua hatua ya kuwatoza watu kodi ya nyumba ya Mungu..Ambayo iliagizwa katika torati na Musa..(2Nyakati 24:9)
Hivyo akawateuwa Walawi, walisimamie jambo hilo tangu mwanzo hadi mwisho, lakini likawa kama linacheleweshwa…
Mpaka baadaye akawauliza tena, kwanini kazi inacheleweshwa, kwa kuona hakuna chochote kilichofanyika..
Lakini mfalme akaja na mkakati mwingine, ili shughuli hiyo ifanyike kwa haraka na wakati, akaona kuliko Kuwalazimisha watu kulipa kodi ngoja aweke sanduku kubwa katika lango la hekalu na kupiga panda kwa watu wote wa Yuda waje kumtolea Mungu wao kwa hiari, bila shuruti..
Na wazo lile likapendwa na watu wengi, na hatma yake makusanyo yakawa mengi, kila siku mpaka wakapata fedha za kuwaajiri wajenzi ili kulikarabati hekalu, na kutengeneza vyombo vya nyumba ya Mungu.
2 Mambo ya Nyakati 24:6-14
[6]Mfalme akamwita Yehoyada mkuu wao, akamwambia, Mbona hukuwataka Walawi waitoze Yuda na Yerusalemu kodi ya Musa mtumishi wa BWANA, na ya kusanyiko la Israeli, kwa ajili ya hema ya ushuhuda?
[7]Kwa kuwa wana wa Athalia, yule mwanamke mwovu, walikuwa wameibomoa nyumba ya Mungu; na vitakatifu vyote vya nyumba ya BWANA wamewapatia mabaali.
[8]Basi mfalme akaamuru, nao wakafanyiza kasha, wakaliweka nje langoni pa nyumba ya BWANA.
[9]Wakapiga mbiu katika Yuda na Yerusalemu, kumletea BWANA kodi aliyoiweka Musa mtumishi wa Mungu, juu ya Israeli jangwani.
[10]Wakafurahi maakida wote na watu wote, wakaleta na kutia ndani ya kasha, hata wakaisha.
[11]Ikawa wakati walipoletewa kasha wasimamizi wa mfalme kwa mkono wa Walawi, nao wakaona ya kwamba kuna fedha nyingi, huja karani wa mfalme, na msimamizi wake kuhani mkuu, wakatoa yaliyomo kashani, kisha hulichukua kasha, na kulirudisha mahali pake. Ndivyo walivyofanya siku kwa siku, wakakusanya fedha tele.
[12]Na mfalme na Yehoyada waliwapa hao waliofanya kazi ya utumishi wa nyumba ya BWANA; nao wakawaajiri waashi na maseremala ili kuitengeza nyumba ya BWANA, na hao pia wafuao chuma na shaba ili kuitengeza nyumba ya BWANA.
[13]Hivyo mafundi wakafanya kazi yao, nao wakaimaliza, wakaisimamisha nyumba ya Mungu kama ilivyopasa, wakaifanya imara.
[14]Nao walipokwisha, wakaleta mbele ya mfalme na Yehoyada fedha iliyobaki, vikafanyizwa kwayo vyombo vya nyumba ya BWANA, vyombo vya utumishi, navyo vya kutolea, na miiko, na vyombo vya dhahabu na fedha. Wakatoa sadaka za kuteketezwa katika nyumba ya BWANA, daima, siku zote za Yehoyada.
Utoaji wenye baraka na anaouhitaji Mungu ni ule wa hiyari na sio wa kulazimishwa…kama kanisa la Kristo Lazima tufikie hatua hii, kwamba viongozi hawawashurutishi watu kutoa mchango,mfano Zaka, Kama vile himizo la kodi, kwamba usipotoa unachukuliwa sheria ya kinidhamu …lakini pia watu nao wanawajibika wenyewe kumtolea Mungu kwa uaminifu na moyo..kanisa lifikiapo hatua hii ya kiroho, Mungu huliongezea baraka sana.
Usikubali kukumbushwa-kumbushwa, au kuhimizwa-himizwa kumtolea Mungu, Bali mtolee Mungu zaka zako, sadaka zako, kwa moyo wa furaha, Bwana atakubariki.
2 Wakorintho 9:6-8
[6]Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.
[7]Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.
[8]Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;
Bwana awabariki..
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/07/21/hekima-iliyo-sahihi-katika-himizo-la-utoaji-sadaka/
Copyright ©2025 Wingu la Mashahidi unless otherwise noted.