TUTAFUTE KWA BIDII KUKAA NDANI YA YESU.

by Devis | 26 July 2025 08:46 am07

Kwa haraka ni rahisi kutafsiri maana ya kukaa ndani ya Yesu ni “kumpokea Yesu”  au “kuishi maisha ya wokovu”..sio makosa kufikiri hivyo kwani ni sahihi kabisa..

lakini leo nitaka tuone maana ya ndani ya “kukaa ndani ya Yesu”.

Awali ya yote hebu kwanza turejee maandiko.

Yohana 15:7 “Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.

Je umeshawahi kumweka mtu moyoni kwa tendo zuri alilokufanyia?..

Au je umeshawahi kumtoa mtu moyoni kwa tendo baya alilokufanyia?.

Kama umeshawahi kupitia mojawapo ya hizo hali basi utakuwa umeshaanza kuelewa maana ya maneno hayo Bwana YESU aliyoyasema kwamba “kaeni ndani yangu nami ndani yenu…(Yohana 15:4).

Maana yake kuna mambo unaweza kuyafanya ukawa umeingia moyoni mwa Kristo, akavutiwa nawe zaidi, ukawa upo moyoni mwake..

Wapo watu ambao Yesu yupo mioyoni mwao (ndani yao) lakini wenyewe hawapo ndani ya YESU.

Hebu tujifunze zaidi kwa mifano…

Unaweza kuwa na marafiki wawili mmoja yupo moyoni mwako sana (aidha kutokana na jambo zuri alilowahi kufanya kwako) na mwingine ni rafiki tu wa kawaida kwako hayupo ndani yako,

Na kuna watu yawekana ukawa mioyoni mwao, lakini wewe usiwe mioyoni mwao..

Na ni hivyo kwa Bwana, kuna watu wapo ndani ya Yesu na kuna ambao hawapo ndani ya Yesu ingawa wamemwamini Yesu.

Sasa swali la msingi, ni kitu gani tunachoweza kufanya kikatuingiza ndani ya moyo wa Bwana YESU, (yaani tukamvutia sana hata kutuingiza ndani yake?).

Majibu ameyatoa yeye mwenyewe Bwana Yesu.

Yohana 6:56 “Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake.

57 Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi”.

Meza ya Bwana  ni tendo moja linalougusa moyo wa Bwana Yesu kuliko tunavyodhani kamwe usipuuzie ushirika mtakatifu.

Jambo la pili linalotuingiza ndani ya YESU, ni Kuzishika amri zake..

1 Yohana 3:24 “Naye azishikaye amri zake hukaa ndani yake yeye naye ndani yake. Na katika hili tunajua ya kuwa anakaa ndani yetu, kwa huyo Roho aliyetupa”

Na amri kuu ni Upendo..

2 Yohana 1:5 “Na sasa mama, nakuomba, si kwamba nakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo, kwamba tupendane.

6 Na huu ndio upendo tuenende kwa kuzifuata amri zake. Hii ndiyo ile amri, kama mlivyosikia tangu mwanzo kwamba mwenende katika hiyo”.

Kwahiyo kwa kufanya mambo mawili makuu, yaani Ushirika wa meza ya Bwana na tukipendana sisi kwa sisi, tutaugusa pakubwa sana moyo wa Kristo.

Na matokeo ya kuwa ndani ya Yesu kwa kufanya mambo hayo mawili, na kupewa chochote tunachokiomba..

Yohana 15:7 “Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa”.

 Mwisho: hatua za kukaa ndani ya Yesu kwanza zinaanza kwa wewe kumpokea Yesu, na ndipo mambo hayo mawili yanafuata.

Je umempokea Yesu kweli kweli?, kama bado unasubiri nini?…mpokee Yesu leo, ufanyike kiumbe kipya na kuoshwa dhambi zako.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/07/26/tutafute-kwa-bidii-kukaa-ndani-ya-yesu/