Je Ayubu alitoka kwenye ukoo gani?

by Nuru ya Upendo | 11 September 2025 08:46 am09

Tofauti na Ibrahimu, Isaka na Yakobo ambao chimbiko lao linaonekana katika mtiririko wake tokea Adamu mpaka Nuru hadi wao wenyewe..

Ayubu yeye ni tofauti, kwani kitabu kinaanza kwa kumweleza yeye, na mahali tu alipokuwa ambapo ni Usi.

Usi ni nchi ambayo ilikuwa nje ya Israeli, maeneo ya aidha Arabia, Syria au Yordani..lakini eneo sahihi kwa uhakika halijulikani hivyo  hakuwa na chimbuko lolote la kiyahudi ndani yake.

Maandiko yanamtaja tu kama “Mtu”, wala sio nabii, au kuhani bali mtu aliyekuwa mkamilifu na mwelekezo aliyemcha Mungu na kuepukana na uovu.

Ayubu 1:1

[1]Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu.

kwanini Mungu aruhusu, watu kama hawa ambao hawakuwa katika mtiririko wa kifamilia waandikwe kwenye biblia na zaidi hata wawe na sehemu kubwa katika ufalme wa Mungu…

Ni kuonyesha kuwa Mungu hana upendeleo, yeyote yule amchaye yeye hukubaliwa naye..ndicho Petro alichokiona kwa Kornelio akasema..

Matendo ya Mitume 10:34-35
[34]Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo;

[35]bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye.

Mwanamke Ruthu hakuwa myahudi, lakini Bwana alimkubali.

Hata na wewe kitendo cha kutozaliwa familia ya kikristo au kichungaji haimaanishi kuwa wewe huna neema ya kumtumikia Mungu. Hapana..ukionyesha bidii ile ile wanayoonyesha wengine Mungu hukujalizilisha neema Izidiyo haijalishi ukoo wenu wote ni wa kiganga. Kila mmoja wetu ana nafasi sawa mbele za Mungu, haijalishi kama ni myahudi au mwarabu, kama ni mzungu au mwafika wote kwa Mungu wanayo neema sawa kwasababu yeye haangalii chimbuko wala sura ya mtu.

Je unamcha Mungu?

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.


DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/09/11/je-ayubu-alitoka-kwenye-ukoo-gani/