by Nuru ya Upendo | 29 September 2025 08:46 am09
SWALI: Tumekuwa tukisikia kuwa mtu akifa, huko aendako anakutana na mateso makali ya jehanamu. Sasa napenda kufahamu je ni roho ndio itakayoteketezwa au na miili pia?
JIBU: Maandiko yanatueleza siku ya mwisho ya hukumu, wafu wote watafufuliwa. (Iwe ni wema au waovu), wote watairudia miili yao ya asili yaliyokuwa nayo duniani.
Yohana 5:28
28 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.
29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu
Ufunuo 20: 12-13
12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.
13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake
Waliokufa katika Kristo (Watakatifu) watavikwa miili mipya ya utukufu, isiyoharibika (1Wakorintho 15:42-54) lakini waovu watakuwa na miili yao ya asili. Ambayo katika hiyo watahukumiwa na kutupwa katika lile ziwa la moto, lililo maalumu kwa mateso ya mtu milele.
Hivyo ni vizuri ifahamike, kuwa kitakachoteketezwa sio roho tu, bali na mwili pia, Bwana Yesu aliliweka hilo wazi katika maneno haya;
Mathayo10:28 Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum.
Umeona hapo?.. Awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum. Kuonyesha kuwa mwili nao utashiriki mateso ya milele.
Tukishayajua hayo, tunapaswa tufanyaje?
Je! Umemwamini Bwana Yesu ndugu? Wokovu ni sasa, mgeukie akuponye, uwe salama, hata ukifa uwe na uhakika wa kuurithi uzima wa milele, Itakufaidia nini kuupata ulimwengu mzima, kisha upate hasara ya nafsi yako? Fanya uamuzi wa busara.
Okoka, leo uponywe. Ikiwa upo tayari kufanya hivyo, basi fungua hapa kwa mwongozo wa sala ya Toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
MWOMBENI BWANA WA MAVUNO APELEKE WATENDA KAZI.
MAUTI NA KUZIMU ZIKAWATOA WAFU WALIOKUWAMO NDANI YAKE.
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/09/29/je-kitakachoadhibiwa-kwenye-ziwa-la-moto-ni-mwili-au-roho-ya-mtu/
Copyright ©2025 Wingu la Mashahidi unless otherwise noted.