Mtambo/mitambo ni nini kibiblia?

by Nuru ya Upendo | 8 October 2025 08:46 pm10

Mtambo kwenye biblia ni neno linalomaanisha aidha kifaa kinachonasa kitu, au kinachorahisisha kazi Fulani.

Kwamfano tukisoma

Ayubu 18:9

[9]Tanzi litamshika kisigino chake,  Na mtambo utamgwia.

Hapo ni Bildadi rafiki yake Ayubu anaeleza hatma ya mtu mwovu, anasema ni sawa na mtu atembeaye katika njia ya mitego, na ghafla hunaswa asiweze kunasuka ndio mtu mwovu katika njia zake mbaya hukumbwa na hayo.

Anasema mtambo utamgwia, maana yake kitu kinasacho Kitamkamata.

Neno hilo pia utalisoma…kwenye mistari ya juu yake..Bildadi anasema..

Ayubu 18:2

[2]Je! Hata lini utayategea maneno mitambo?  Fikiri, kisha baadaye tutanena.

Akitumia lugha ya picha…

akimaanisha hata lini utayanasa maneno yako? (yaani utaacha kuongea?).

Lakini sehemu nyingine Inayolitaja Neno hili Ni..

2 Mambo ya Nyakati 26:14-15

[14]Uzia akawafanyizia jeshi lote ngao na mikuki, na chapeo, na deraya za madini, na nyuta, na mawe ya kupiga kwa teo.

[15]Akafanya katika Yerusalemu mitambo ya vita, iliyobuniwa na watu wastadi, iwekwe juu ya minara na juu ya buruji, ili kutupa mishale na mawe makubwa. Jina lake likaenea mbali sana; kwa kuwa alisaidiwa mno ajabu, hata akapata nguvu.

Inazungumzia nguvu za kijeshi alizokuwa nazo mfalme Uzia, hata kufikia kubuni mitambo mikubwa ya kivita.. ya kufyatulia silaha kwa maadui zake.

Bwana akubariki

Je umeokoka?

Kumbuka saa Tulizopo ni za majeruhi, siku yoyote wakati wowote Kristo anarudi jiulize umejiandaaje ndugu?. Unyakuo wa kanisa ukipita leo utakuwa wapi mpendwa…

Jitathmini maisha yako? Itakufaidia nini uupate ulimwengu wote na mambo yake halafu upate Hasara ya nafsi yako. Tubu mgeukie Kristo uoshwe dhambi zako, upokee uzima wa milele.

Ikiwa upo tayari kumpokea Yesu leo.. basi fungua hapa kwa mwongozo Wa Sala ya Toba.. >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/10/08/mtambo-mitambo-ni-nini-kibiblia/