Dhuluma/Kudhulumu ni nini kibiblia (Mathayo 6:11)?

by Nuru ya Upendo | 20 October 2025 08:46 am10

Jibu: Turejee..

Mwanzo 6:11 “Dunia ikaharibika mbele za Mungu, dunia IKAJAA DHULUMA.

12 Mungu akaiona dunia, na tazama, imeharibika; maana kila mwenye mwili amejiharibia njia yake duniani.

13 Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia dhuluma, basi nitawaharibu pamoja na dunia”.

Kwa tafsiri ya Kawaida Dhuluma/kudhulumu ni kitendo cha kumnyima au kumpokonya mtu haki yake kwamfano kwamfano umeazimwa pesa na haujairudisha na unao uwezo wa kufanya hivyo,  hiyo ni dhuluma.

Au mtu ana haki ya kupata huduma fulani kutoka kwako na humpatii kwasababu binafsi hapo unakuwa unamdhulumu haki yake.. Na dhuluma ya namna hii ni dhambi..

Lakini katika Biblia neno hili Dhulumu limeenda mbali zaidi likijumuisha mambo mengi zaidi ya “kumnyima tu mtu haki yake” bali limejumisha pia “vurugu, uonevu, ubaya na uasi”.

Hivyo Neno dhuluma linapotajwa kwenye Biblia linabeba maana pana zaidi ya tunayoifahamu na kuitumia sasa.. Kwamfano hapo katika Mwanzo 6:11-13 inapotajwa Dhuluma, imemaanisha vitendo vyote vya vurugu, uonevu, maasi, na kuwanyima watu haki zao, na hiyo ndio ikawa sababu ya Mungu kuigharikisha Dunia ya kwanza..

Mwanzo 6:11 “Dunia ikaharibika mbele za Mungu, dunia IKAJAA DHULUMA.

12 Mungu akaiona dunia, na tazama, imeharibika; maana kila mwenye mwili amejiharibia njia yake duniani.

13 Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia dhuluma, basi nitawaharibu pamoja na dunia”.

Maandiko mengine yanayotaja dhuluma ni pamoja na Zaburi 55:9-11, Zaburi 82:2, Zaburi 119:78, Zaburi 119:134, Warumi 2:8 na Ufunuo 22:11.

Je umempokea YESU?.. au upo bado unatanga tanga na dhuluma za huu ulimwengu?.. Kumbuka maandiko yanasema Dunia ya kwanza iligharikishwa kwa maji lakini hii ya sasa imewekwa akiba kwa moto, kwasababu zile zile zilizoigharikisha Dunia ya kwanza (yaani ya kipindi cha Nuhu).

2Petro 3:6 “kwa hayo dunia ile ya wakati ule ILIGHARIKISHWA NA MAJI, ikaangamia.

7 Lakini mbingu za sasa na nchi ZIMEWEKWA AKIBA KWA MOTO, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu”.

Bwana YESU mkuu wa haki  (Zaburi 45:7) ANARUDI!

Maran atha!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

WhatsApp
DOWNLOAD PDF

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/10/20/dhuluma-kudhulumu-ni-nini-kibiblia-mathayo-611/