by Nuru ya Upendo | 20 October 2025 08:46 pm10
Jibu: Turejee..
Matendo 5:16 “Nayo makutano ya watu wa miji iliyoko kandokando ya Yerusalemu wakakutanika, wakileta wagonjwa, nao WALIOUDHIWA NA PEPO WACHAFU; nao wote wakaponywa”.
Katika Biblia, neno “Kuchukizwa” au “Kuchukiza” limekuwa na maana zaidi mbili, maana ya kwanza ya kuchukizwa ni ile hali/hisia ya “Kutopendezwa na jambo” inayozaa huzuri, au hasira mfano wa hiyo ni ile iliyompata Bwana Yesu alipokutana na Sauli alipokuwa anaenda Dameski kuwafunga wakristo..
Matendo 9:3 “Hata alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza kote kote nuru kutoka mbinguni.
4 Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, SAULI, SAULI, MBONA WANIUDHI?
5 Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, MIMI NDIMI YESU UNAYENIUDHI WEWE.
6 Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda”.
Hapa inaonyesha ni jinsi gani matendo ya Sauli ya kikatili yalivyokuwa yanamwudhi Bwana.. Lakini pia tunaona mahali pengine pakionyesha Wayahudi walikuwa wakimwudhi Bwana YESU kwasababu alikuwa anafanya miujiza siku ya sabato..
Yohana 5:14 “Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi.
15 Yule mtu akaenda zake, akawapasha habari Wayahudi ya kwamba ni Yesu aliyemfanya kuwa mzima.
16 Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwudhi Yesu, kwa kuwa alitenda hayo siku ya sabato.
17 Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi”
Sasa si mahali pote katika Biblia neno hilo “kuudhi/kuudhiwa” limemaanisha “kukwazwa au kutopendezwa na jambo fulani” bali sehemu nyingine limemaanisha “KUTESWA”
Mfano wa sehemu hizo ni hapa katika kitabu cha Matendo ya Mitume..
Matendo 5:16 “Nayo makutano ya watu wa miji iliyoko kandokando ya Yerusalemu wakakutanika, wakileta wagonjwa, nao WALIOUDHIWA NA PEPO WACHAFU; nao wote wakaponywa”
Kuudhiwa kunakomaanishwa hapo ni ile hali ya “Kuteswa na Kuonewa” Hivyo hapo Biblia imemaanisha kuwa waliokuwa wanateswa na pepo wachafu walifunguliwa, hali kadhalika mahali pengine panapoonesha kuwa kuudhiwa kunakomaanisha kuteswa ni katika kitabu kile cha Ufunuo 12:13.
Ufunuo 12:13 “Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume”.
Na katika Mathayo 5:10-12 ni Maudhi ya Mateso yanayozungumziwa hapo..
Mathayo 5:10 “Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
11 Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu.
12 Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu”
Je na wewe unaudhiwa kwaajili ya haki au kwaajili ya Mabaya?…Kama ni kwaajili ya Kristo basi fahamu kuwa thawabu yako ni kubwa mbinguni, lakini kama ni kwaajili ya mabaya, basi tubu leo na mpokee YESU akutoe katika hizo dhiki ambazo hazina faida yoyote bali mwisho wake ni hasara mara mbili katika siku ile ya mwisho.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/10/20/pepo-waliwaudhi-vipi-watu-matendo-516/
Copyright ©2025 Wingu la Mashahidi unless otherwise noted.