Kutawa ni nini? Sawasa na Luka 1:24

by Nuru ya Upendo | 3 November 2025 08:46 pm11

Swali: Kutawa kwa Elisabeti miezi mitano maana yake nini?


Jibu: Turejee..

Luka 1:24 “Hata baada ya siku zile mkewe Elisabeti alichukua mimba AKATAWA miezi mitano, akisema,

25 Hivi ndivyo alivyonitendea Bwana katika siku zile alizoniangalia ili kuniondolea aibu yangu mbele ya watu”.

Tafsiri ya “Kutawa” ni “kujitenga”.. hivyo Kiswahili kingine cha mstari huo ni hiki… “Hata baada ya siku zile mkewe Elisabeti alichukua mimba AKAJITENGA miezi mitano”

Hivyo Elisabeti alijitenga na jamii ya watu pengine kwasababu za kumshukuru MUNGU kwa muujiza aliomtendea wa kubeba mimba uzeeni, au kwa nia ya kuepusha uadui kutoka kwa watu ambao ungetokana na wivu, au pengine kwasababu nyingine za kupumzika na kumtafakari MUNGU kwa faragha!. Mojawapo ya hizo au zote zaweza kuwa sababu za kujitenga kwake.

Na tunaona lilikuwa ni jambo jema kwa Elisabeti kwani baadaye alipokutana na Mariamu ndugu yangu, alijazwa Roho Mtakatifu na kuzungumza  kiusahihi habari za Mariamu na Bwana Yesu aliye tumboni mwa Mariamu.

Hiyo inatufundisha nini?

Si kila Baraka kutoka kwa MUNGU inapokuja ni wakati wa kutangaza na kushuhudia wakati huo huo, wakati mwingine ni vizuri kujitenga/kutawa kwa muda ili kutumia kumshukuru MUNGU, na kuomba ulinzi wa Baraka ile,..kuwahi kutangaza Baraka za MUNGU au mlango MUNGU aliokufungulia kabla ya kupata utulivu ni hatari kwako na kwa utakaoenda kuwaambia.

Hivyo ni vizuri kutokuwa mwepesi wa kuzungumza bali ni vizuri kuwa mwepesi wa kupata faragha na MUNGU na kutafakari fadhili zake kabla ya kuzungumza au kushuhudia.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MARIAMU AKUTANA NA ELISABETI.

Yohana aliwatiaje waasi akili za wenye haki? (Luka 1:17)

KWA VILE ALIVYOKUWA MTU WA HAKI.

JE BIKIRA MARIAMU ALIZAA WATOTO WENGINE?

UWEZA WA MUNGU UNAONEKANA WAPI?

WhatsApp
DOWNLOAD PDF

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/11/03/kutawa-ni-nini-sawasa-na-luka-124/