BWANA NISAIDIE, KUTOKUAMINI KWANGU

by Nuru ya Upendo | 9 November 2025 08:46 pm11

Marko 9:24

[24]Mara babaye yule kijana akapaza sauti, akasema, Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu.

Habari ya yule mzee ambaye kijana wake alivamiwa na mapepo sugu ya kumtupa motoni tangu utoto wake, na baada ya kuhangaika sana kwa madaktari na kila aina ya matabibu, hadi mitume nao kushindwa kumponya, hatimaye akakutana na Bwana Yesu..

Akamwambia ‘Ukiweza’ Bwana neno utuhurumie na kutusaidia… lakini saa hiyo Hiyo Yesu akamjibu….Ukiweza?..

Mimi unaniambia ukiweza?

Marko 9:23

[23]Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye.

Kuonyesha kuwa Imani yake, haikuwa kamili, lakini, saa hiyo hiyo akaweka tegemeo lake lote kwa Yesu na kumwamini..’Naamini’…lakini pia nisaidie ‘kutokuamini kwangu’..

Hiki ni Moja ya ombi ya uwazi na la ukweli kabisa ambalo tunaweza kulisoma kwenye biblia…

Ni kweli ameamini, lakini imani yake si timilifu, anapambana sana kuifanya iwe sawa.. hivyo pamoja na hilo akamwona na Bwana amsaidie…kuonyesha tabia ya kujiachia kikamilifu kwa Bwana…kwamba sio tu kutendewa muujiza lakini pia kusaidiwa..

Saa hiyo hiyo Yesu hakumfukuza, wala kumkemea, wala kumwambia kafanye hivi au vile kwanza… bali akamkemea yule pepo Na hatimaye kijana akawa mzima saa ile ile.

Imani, ya kweli haimaanishi kwamba mashaka yatapotea…bali ni kuchagua kujimimina kwa Bwana na kuweka tegemeo lako lote kwake tu, hata kama moyo wako utakuambia wewe mbona unamashaka mashaka, mbona huna imani, mbona maneno yako mwenyewe yanathibitisha umekata tamaa..

Hakika hapo usiache kuomba na kukiri, ukiulilia pia msaada wa Bwana akusaidie imani yako iwe Kamilifu, kwa kujimimina tu hivyo hatimaye utayaona mambo makubwa akikutendea..

Usianze kujilaumu kwa mashaka mia uliyoonyesha, wewe egemea tu kwa Yesu bila kuondoa mguu wako hapo…atakujenga..Yule baba hakuondoka kwa Yesu, kwasababu ya madhaifu yake bali aliendelea kukaa pale pale. Kwasababu imani inajengwa kwa mahusiano sio kwa utimilifu wetu.

neema ya Mungu hizidi mapungufu yetu..kiri.udhaifu wako kwake, lakini onyesha kumtegemea yeye, hapo nguvu za Mungu utaziona.

Shetani atataka ujilaumu, katika shida yoyte lakini sema…

“Naamini, Bwana, nisaidie kutokuamini kwangu.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

JAWA SANA MOTO ULAO.

ENDELEZA UPONDAJI.

MBONA MMESIMAMA HAPA MCHANA KUTWA BILA KAZI?

WhatsApp
DOWNLOAD PDF

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/11/09/bwana-nisaidie-kutokuamini-kwangu/