BABA AKIMBIAYE

by Nuru ya Upendo | 10 November 2025 08:46 pm11

Luka 15:20

[20]Akaondoka, akaenda kwa babaye. Alipokuwa angali mbali, baba yake alimwona, akamwonea huruma, akaenda mbio akamwangukia shingoni, akambusu sana. 

Habari ya mwanampotevu hufunua picha halisi ya rehema na huruma nyingi za Mungu kwetu. Baada ya yule mwana mdogo, kupoteza kila kitu, kwa maisha ya anasa..mwishowe alizingatia kurudi kwa baba yake, Akiwa na fikra za aidha kulaumiwa, Kutengwa, au pengine kuadhibiwa na kufanywa mtumwa…lakini mambo yalikuwa mbali sana na mategemeo yake..tena sanaa..

Kabla hata hajamwona Baba yake, Baba yake alishamwona kwanza yeye kwa mbali… lakini si hilo tu, mzee yule hakungoja kijana wake amfikie, bali alitoka saa ile ile akaanza kukimbia kumwelekea mwana wake..

Hilo jambo La ajabu sana, kwani kwa tamaduni za zamani, hata sasa…mtu mzima kukimbia, Ni aidha kuna jambo la taharuki sana…au la hisia kubwa kupita kiasi…kwasababu watu wazima hawakimbii ovyo..

Lakini kwa huyu mzee, ilibidi akaidi kanuni hiyo..akimbie kama mtoto mdogo kumwelekea mwanawe na alipomfikia akamkumbatia na kumbusu sana…unaweza tengeneza picha ni hisia gani kali yule baba alikuwa nazo kwa mwanawe..

Mambo kama hayo ni rahisi kuyaona kwa mzazi ambaye pengine mtoto wake ampendaye alikuwa amesafiri kwa wakati mrefu na sasa amekuja kumsalimia Nyumbani…lakini si rahisi kuona mzazi anaonyesha hivyo kwa mtoto mtukutu, mwenye kiburi, aliyeshindikana…pengine angemkaribisha tu, na kumsamehe, na kuongea naye kawaida…lakini huyu alichinjiwa mpaka mnyama na karamu juu..

Hii ni habari inayofunua hisia za Mungu kwa mwenye dhambi atubupo kwa dhati…

Kabla Hata hujamaliza ombi la toba tayari Mungu ameshakukimbilia na kukukumbatia, neema yake ya kusamehe inazidi wingi wa dhambi tulizomtenda…

Yawezekana wewe umekuwa mwana mpotevu kwa kurejea kwenye Dhambi ambazo ulishaziacha zamani…vipi kama ukitubu leo kwa kumaanisha.?

Ulitoka nje ya ndoa Yako…tubu sasa…ulirudia tabia ya uzinzi na kujichua..tubu sasa, Umerudia ulevi na anasa..embu tubu..Mungu yupo tayari kukukimbilia…Na kukusamehe zaidi ya matarajio yako.

Na kukusaidia…yule mwana mpotevu “alizingatia” embu na wewe zingatia pia leo.. kuacha hayo maisha ya kale…haijalishi umefanya makosa Mengi ya aibu namna gani..Tubu tu leo na kutupa hivyo vikoba vya kiganga, na ufiraji, na wizi na rushwa uzifanyazo. na Bwana atakuponya.

Kumbuka ukifa katika dhambi zako ni moja kwa moja kuzimu..kwanini iwe hivyo wakati akusameheaye anakukimbilia?

Usimzuie, achilia akili zako mrudie muumba wako.

Bwana akubariki.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>

https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

BWANA NISAIDIE, KUTOKUAMINI KWANGU

JAWA SANA MOTO ULAO.

TENGENEZA NJIA YAKO.

WhatsApp
DOWNLOAD PDF

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/11/10/baba-akimbiaye/