USHUHUDA WA MATENDO NI MKUU KULIKO WA MANENO.

by Nuru ya Upendo | 13 November 2025 08:46 pm11

Jina la Bwana YESU KRISTO libarikiwe, karibu tujifunze Biblia Neno la MUNGU wetu lililo Taa na Mwanga wa njia  yetu (Zab. 119:105).


“Maneno” yanafaa kuthibitisha jambo, lakini “matendo” ni bora zaidi.. Hebu tujifunze kwa Bwana YESU ambaye alitumia matendo zaidi kuliko maneno.

Kipindi ambacho  Yohana Mbatizaji anawatuma wanafunzi wake kwa YESU kumwuliza kama yeye ndiye au wamtazamie mwingine, jibu la YESU halikuwa “Ndio mimi ndiye”.. bali aliwaambia wale watu wamrudie Yohana wamwambie wanayoyaona, viwete wanatembea, vipofu wanaona..

Mathayo 11:2 “Naye Yohana aliposikia huko gerezani matendo yake Kristo, alituma wanafunzi wake, kumwuliza,

3 Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine?

4 Yesu akajibu akawaambia, Nendeni mkamweleze Yohana mnayoyasikia na kuyaona;

5 vipofu wanapata kuona, viwete wanakwenda, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa habari njema”.

Umeona hapo KRISTO hakutumia maneno kujieleza yeye ni nani bali matendo.. Kwa ufupi kazi zake zilimshuhudia yeye ni nani, na sio hapo tu bali kila mahali ilikuwa ni hivyo hivyo..

Yohana 10:24 “Basi Wayahudi walimzunguka, wakamwambia, Hata lini utatuhangaisha nafsi zetu? Kama wewe ndiwe Kristo, utuambie waziwazi.

25 Yesu akawajibu, Naliwaambia, lakini ninyi hamsadiki. Kazi hizi ninazozifanya kwa jina la Baba yangu ndizo zinazonishuhudia”.

Umeona, kumbe kazi (yaani matendo) ya YESU ndio yaliyomshuhudia??…  Je na sisi tutumie kipi kutangaza ushuhuda wetu?.. maneno yetu au kazi zetu?..Bila shaka Matendo yetu yanafaa zaidi kuliko maneno.

Tutatambulika kuwa sisi ni wakristo kwa matendo na si maneno tu.. tutatambulika sisi ni watumishi kwa matendo na si maneno matupu tu!, tutatambulika sisi ni wakweli kwa matendo na si kwa maneno tu.

Ukisema umepata badiliko moyoni, uthibitisho wa badiliko hilo ni matendo ya mwilini, kwamba kama umebadilishwa tabia basi huwezi kuendelea kuiba, au kutukana au kuvaa vibaya au kufanya uzinzi, uthibitisho wa badiliko la ndani ni matendo ya nje, na si maneno tu..

Mathayo 5:16 “Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni”.

Hivyo tutie bidii kutengeneza matendo yetu zaidi ya maneno yetu.

Bwana YESU atusaidie..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MAISHA ULIYOPITIA NYUMA NI USHUHUDA TOSHA WA WEWE KUMTUMIKIA MUNGU

ENDELEZA UPONDAJI.

USHUHUDA WA RICKY:

MBONA MMESIMAMA HAPA MCHANA KUTWA BILA KAZI?

MWIMBIE BWANA ZABURI KATIKA NYAKATI ZA FURAHA.

WhatsApp
DOWNLOAD PDF

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/11/13/ushuhuda-wa-matendo-ni-mkuu-kuliko-wa-maneno/