Je? ni sahihi kwa watu wa MUNGU kutumia majina ya wanyama kuwaita wengine.

by Nuru ya Upendo | 18 November 2025 08:46 pm11

SWALI:Je? ni sahihi kwa watu wa MUNGU kutumia majina ya wanyama kuwaita wengine.mfano “We kenge njoo hapa”, kama YESU alivyo tumia mbweha katika

luka 13:32.


JIBU: Katika biblia tunaona watu wakiitwa kwa majina mbalimbali ya wanyama mfano mbwa mwitu (Mathayo 7:15), kondoo(Yohana10:27), nyoka(Mathayo 13:34). Lakini pia mbweha, Njiwa, nguruwe, Simba, mbuzi.

Sasa ni vema kufahamu makusudio ya watu/jamii kuitwa hivyo yalikuwa ni nini, hayakuwa kwa lengo la kutukana, au kukejeli, au kudharau..

Hapana Bali kwa lengo la kuonyesha tabia ya mtu, jinsi ilivyo hilo tu.

Kwamfano Yesu alipomuitwa Herode Mbweha, hakuwa na kusudi la kumtukana, au kumdharau, bali alikuwa Anaeleza tabia zake zilizo mfano wa mbweha, ambaye anatabia ya kuvizia na kurarua wanyama wadogo na kuwaua. Maana hivyo ndivyo Herode alivyokuwa, jambo lililoonekana Hata kwa baba zake Kipindi Yesu anazaliwa walimwinda ili wamuue.

Sasa Ikiwa mtu atajulikana kwa namna kama hiyo, kibiblia sio tusi.

Lakini kinyume chake watu hutumia Majina ya wanyama kuwatukana Wengine, au kuwaabisha, au kuonyesha dharau kinyume chao, chuki au hasira, hayo biblia imekataza…na ni dhambi

Kusema “wewe kenge njoo hapa”..Moja kwa moja kauli hiyo inaonyesha chanzo chake ni hasira, dharau au chuki.

Waefeso 4:29

[29]Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia. 

Wakolosai 3:8

[8]Lakini sasa yawekeni mbali nanyi haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano, na matusi vinywani mwenu. 

Mathayo 5:22

[22]Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto. 

Hivyo chunga kinywa chako. Kila Neno ulisemalo pima makusudi yaliyo nyuma yake.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

VILIO VINAVYOUFIKIA MOYO WANGU.

 

JAWA SANA MOTO ULAO

USIWAOGOPE WAZAMZUMI

WhatsApp
DOWNLOAD PDF

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/11/18/je-ni-sahihi-kwa-watu-wa-mungu-kutumia-majina-ya-wanyama-kuwaita-wengine/