Lile vazi lenye wanyama najisi liliwakilisha nini? (Matendo 10:9-15)

by Nuru ya Upendo | 16 December 2025 08:46 am12

Swali: Je! lile shuka la wale wanyama najisi, Mtume Petro aliloliona likiteremshwa kutoka mbinguni katika Matendo 10:9-15 liliwakilisha nini?..

Jibu: Turejee….

Matendo 10:9-15 “Hata siku ya pili, walipokuwa wakisafiri na kuukaribia mji, Petro alipanda juu darini, kwenda kuomba, yapata saa sita ya mchana; 

10 akaumwa na njaa sana, akataka kula; lakini walipokuwa wakiandaa, roho yake ikazimia, 

11 akaona mbingu zimefunuka, na chombo kikishuka kama nguo kubwa, inatelemshwa kwa pembe zake nne hata nchi; 

12 ambayo ndani yake walikuwamo aina zote za wanyama wenye miguu minne, na hao watambaao, na ndege wa angani. 

13 Kisha sauti ikamjia, kusema, Ondoka, Petro, uchinje ule.

14 Lakini Petro akasema, Hasha, Bwana, kwa maana sijakula kamwe kitu kilicho kichafu au najisi. 

15 Sauti ikamjia mara ya pili, ikimwambia, Vilivyotakaswa na Mungu, usiviite wewe najisi”

Katika Ono hili, wale wanyama najisi aliowaona katika ile nguo, ni “Watu wa Mataifa”…Ambao kwaasili ndio waliokuwa wanaonekana najisi mbele za MUNGU, hawakuweza kuwa warithi wa ahadi za MUNGU, wala wahudumu wa utumishi wa MUNGU.

Lakini hapa Bwana MUNGU alikuwa anaongea na Petro kwa njia ya Ono kuwa Mataifa sio najisi tena mbele za MUNGU, hivyo Petro asiogope kuwapelekea Injili.

Kwahiyo kwa ufupi wale wanyama najisi  waliwakilisha “Watu najisi qa mataifa”… tunazidi kulithibitisha vipi hilo?..

Tuangalie ule mstari wa 14-15 na ule wa 28..

Matendo 10:14 “Lakini Petro akasema, Hasha, Bwana, kwa maana sijakula kamwe kitu kilicho kichafu au najisi. 

15 Sauti ikamjia mara ya pili, ikimwambia, VILIVYOTAKASWA NA MYNGU USIVIITE WEWE NAJISI” 

………….

28 Akawaambia, Ninyi mnajua ya kuwa si halali mtu aliye Myahudi ashikamane na mtu aliye wa taifa lingine wala kumwendea, lakini Mungu AMENIONYA NISIMWITE MTU AWAYE YOTE MCHAFU WALA NAJISI”.

Kwahiyo kwa maneno hayo ya Petro ni wazi kuwa alipewa ufunuo na Roho Mtakatifu kuwa wale wanyama najisi aliowaona ni watu ambao wao walikuwa wanawaona kama najisi mbele za Mungu (yaani watu wa Mataifa, akiwemo Kornelio na familia yake).

Ikifunua kuwa katika suala la Neema ya MUNGU, hakuna upendeleo kwa mtu yeyote myahudi au asiye myahudi.

Wagalatia 3:28 “Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu”

Lakini pia ni wanyama pia wametakaswa, katika agano jipya hakuna katazo la kula wale wanyama waliokatazwa wakati wa agano la kale, kwani walikuwa wanawakilisha tu aina ya watu, kwa ufupi wanyama walisimama kama ishara ya jamii ya watu, lakini si kwaasili kwamba ni najisi.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

WhatsApp
DOWNLOAD PDF

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/12/16/lile-vazi-lenye-wanyama-najisi-liliwakilisha-nini-matendo-109-15/