Kibiblia mtu asiye na Ufahamu ni “Mjinga”..Na hapa Neno la MUNGU linasema… “Enyi wajinga, acheni ujinga, mkaishi, Mkaende katika NJIA YA UFAHAMU”..
Sasa hiyo sio Kejeli wala Tusi, bali ni onyo, kwamba mtu akiendelea kuishi katika Ujinga atapoteza maisha yake, kwasababu ya kukosa ufahamu.
Sasa swali ni je! Ufahamu ni nini na njia ya ufahamu ni nini?.. Biblia hii hii imetupa majibu ya nini maana ya ufahamu.
Ayubu 28:28 ”Kisha akamwambia mwanadamu, Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima, NA KUJITENGA NA UOVU NDIO UFAHAMU”.
Kumbe mtu anayejitenga na Uovu kwa mujibu wa Biblia ndio mwenye Ufahamu!.
Mtu anayejitenga na zinaa, ulevi, ibada za sanamu, uuaji, uvaaji mbaya n.k ana UFAHAMU!!..
Nilifikiri Biblia ingesema mtu mwenye ufahamu ni yule mwenye elimu kubwa, au mwenye uwezo wa kutafuta Pesa..Lakini kumbe ni kinyume chake.
Mtu awe na elimu kubwa au cheo kikubwa, elimu kubwa au uwezo mwingine wowote wa kimaisha na huku dhambo bado inamshinda ni MJINGA kulingana na Biblia.
Na Biblia imesema “Mjinga aache ujinga wake akaishi”.
Je wewe ni Mjinga au mwerevu?.
Kama bado upo chini ya utumwa wa dhambi, basi kuna ujinga unakusumbua ambao YESU KRISTO anaweza kukusaidia ukatokana nao na ukapata Ufahamu.
Kinachohitajika ni wewe tu kudhamiria kutubu kwa kumaanisha kuacha dhambi, na kubatizwa katika ubatizo sahihi na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
Kuanzia huo wakati Ufahamu wa KiMungu utaingia ndani yako.
Bwana atusaidie.