LAKINI DAUDI ALIJITIA NGUVU KATIKA BWANA, MUNGU WAKE.

by Nuru ya Upendo | 9 February 2026 08:46 pm02

1 Samweli 30:6

[6]Naye Daudi akafadhaika sana; kwa sababu watu walikuwa wakisema kwamba apigwe kwa mawe, kwa maana nafsi za hao watu wote walisononeka, kila mtu kwa ajili ya wanawe na binti zake; lakini Daudi alijitia nguvu katika BWANA, Mungu wake. 

Zipo nyakati, ambazo watu wanaokuzunguka wanaweza kufarakana nawe, kama sio watu basi mazingira au hali zinazokuzunguka zinaweza kukupinga kabisa kiasi kwamba ukakata tamaa ya kusimama au kuendelea mbele.. ukiangalia kulia, ukiangalia kushoto hakuna linalokusapoti…si watu, si vitu.

Ndio lililomkuta Daudi, ambaye hapo mwanzo walikuwa wanamwimbia “ameua makumi elfu”, waliyempenda, lakini mambo sasa yamegeuka wanataka kumpiga mawe…afe, 

Hakuona mtu wa kumshika mkono kumwinua au kumfariji…Hivyo na yeye hakukaa chini na kulia na kusema Bwana mbona sioni msaidizi, hakukaa chini na kusema Bwana ona fadhili zote nilizowatendea leo wanataka nipiga mawe, 

Daudi ijapokuwa alikuwa katika mafadhaiko makubwa, maandiko yanatuambia AKAJITIA NGUVU MWENYEWE, katika Bwana..Mungu wake..

Hakutafuta kutiwa nguvu na mtu. Na matokeo yake alipolifuatilia jeshi, akalipata akawapiga, kisha akawarudishia mateka wao wote walioibiwa na mali nyingi..ukawa ushindi mkuu sana.

Lakini hiyo yote ilianza kwa kujitia nguvu mwenyewe ndani. Hayo ndio yalikuwa mafanikio ya Daudi.  

Leo hii watu wengi, wanabakia kusubiri faraja za watu, kuinuliwa na watu, kuthibitishwa na watu…Ni kweli hayo ni vizuri lakini yanapoondoka basi na maono hufia hapo hapo…lakini tukijitia nguvu katika Bwana.. tutafanikiwa katika nyakati zote hata zile ngumu. 

Hatufanikiwi ndipo tujitie nguvu katika Bwana…tunajitia nguvu kwanza ndipo ushindi unakuja, baadaye hiyo ndio kanuni ya kiroho.

Kabla ya mikakati, mipango, tunajitengeneza kwanza wenyewe nafsi zetu, humu ndani, tukimuamini Mungu aliyetuita kuwa ameahidi hatatuacha, wala kutupungukia. Ndipo tunapoelekea kutekeleza maono yetu.

Tembea na kanuni hiyo. Ondoa matarajio kwa wanadamu.

Bwana akubariki

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

WhatsApp
DOWNLOAD PDF

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2026/02/09/lakini-daudi-alijitia-nguvu-katika-bwana-mungu-wake/