KUJITAKASA NI MUHURI WA UTAKATIFU

by Nuru ya Upendo | 28 March 2026 08:46 pm03

Biblia inasema watakatifu waliopo duniani ndio Bwana wanaompendeza.

Zaburi 16:3 “Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao”.

Lakini swali ni je! anaposema “Watakatifu”..anamaanisha ni watu wasiokosea kabisa?…kwamba hawawezi kabisa kufanya makosa na kwamba wamekamilika kwa asilimia zote?.

Jibu ni Ndio! … watu wote waliompokea YESU na kupokea Roho Mtakatifu wamekamilika kwa asilimia zote katika vigezo vya “Kuokolewa”, mbele za Mungu lakini si katika vigezo vya kutokosea kabisa (Yaani kufanya mistakes).

Kukosea kusoma maandiko wakati wa mahubiri hayo ni makosa (mistakes), kusahau kutimiza ahadi uliyoitoa kwa mtu ni makosa..

Sasa makosa ya namna hiyo hayawezi kumpokonya mtu haki ya kuwa “MTAKATIFU” mbele za MUNGU.

Vile vile ikiwa mtu kampokea YESU leo na bado hajajua kuwa “anapaswa akabatizwe” ili akamilishe wokovu wake (sawasawa na Marko 16:16).

Na akawa katika hali hiyo hiyo ya kutobatizwa lakini bado anafanya mengine ya imani yaliyo sahihi bado hiyo haimwondolei sifa ya kuwa MTAKATIFU MBELE ZA MUNGU…yupo miongoni mwa watakatifu wa Bwana waliopo ulimwenguni.

Halikadhalika na mambo mengine yote ambayo mtu hajayajua wala kuyasikia kama ni makosa katika hatua zake za awali za wokovu, hayawezi kumpokonya haki ya kuwa mtakatifu mbele za MUNGU.

Lakini anaposikia au kuujua ukweli na kuupinga au kukataa mabadiliko anapoteza moja kwa moja sifa ya kuwa MTAKATIFU mbele za MUNGU.

Kwa namna gani?

Hebu tusome

Ufunuo 22:1″Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; NA MTAKATIFU NA AZIDI KUTAKASWA

Nataka tuone hapo…“NA MTAKATIFU NA AZIDI KUTAKASWA”..

Kama MTAKATIFU ameshakamilika hafanyi makosa kwanini tena hapo maandiko yaseme…“NA AZIDI KUTAKASWA”..

Kumbe MTAKATIFU bado anaweza KUTAKASWA.

Maana yake ni kwamba hakuna kipimo fulani  maalumu kwamba hapa mtu kashafikia  UTAKATIFU wa mwisho…

UTAKATIFU ni jambo endelevu, kwamba kila siku tunajiona kasoro zetu na kufanya mabadiliko.

Unaweza kujiona leo upo sawa kabisa kiimani na kiutakatifu..lakini baada ya mwezi mmoja uliposoma Neno ukajigundua kuna mambo ulikuwa unakosea hivyo ukajirekebisha,….hapo maana yake “umejitakasa”.

Sasa kipindi ambacho hukuwa unajua makosa, haimaanishi kwamba haukuwa mtakatifu..La! Ulikuwa mtakatifu…

Lakini siku ulipojua jambo fulani ni kosa na kubadilika..hapo “ulizidi kuwa mtakatifu”…na siku utakapojua jambo jingine ambalo leo hii hulijui. Na jambo hilo ukaliacha “hapo utazidi kuwa mtakatifu mara mbili zaidi”.

Kwahiyo ili tuweze kuhesabika ni watakatifu ni lazima “TUJITAKASE”.

Je na wewe ni Mtakatifu?..Je na wewe unajitakasa?.

Swali unajitakasaje?.

Unajitakasa kwa kukaa mbali na kila aina ya vichocheo vya dhambi, na kwa kusoma Neno na maombi pamoja na kukusanyika na wengine (kufanya ibada).

Kuna mambo hutaweza kujua kuwa ni makosa pasipo kusoma Neno, kuna mambo huwezi kujua kuwa ni makosa usipokuwa mwombaji n.k

Bwana akubariki na kuzidi kutusaidia..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

WhatsApp
DOWNLOAD PDF

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2026/03/28/kujitakasa-ni-muhuri-wa-utakatifu/