EPUKA UVUGUVUGU.

by Nuru ya Upendo | 27 April 2026 08:46 am04

Uvuguvugu ni ile ya hali ya  kuchanganya mambo mema na mazuri (mema na mabaya kwa wakati mmoja).. Na roho ya uvuguvugu ilianzia EDENI, ndiyo shetani anayoitumia kuangusha watu.

Kwa namna gani?

Turejee mojawapo ya miti iliyokuwepo Edeni, Biblia inatuambia kulikuwepo na “Mti wa Ujuzi wa MEMA na MABAYA” ambao Bwana MUNGU alitoa maagizo wasiuguse wala kula matunda yake.

Huu ulikuwa ni mti wenye sifa ya UVUGUVUGU, yaani wenye “Mema na Mabaya wakati huo huo”.. Na ibilisi alijua mwanadamu anapenda Uhuru wa kufanya mambo yote kwa pamoja, (mema kidogo na mabaya kidogo).. na alianza kupitisha ushawishi huo kwa Hawa, na pasipo kuzitambua hila za ibilisi, tukaingia katika kosa la moja kwa moja.

Ndugu ibilisi hamtegi mtu wa Mungu (aliyesimama) kwa mabaya.. bali atamtega kwa “Mabaya yaliyochangamana na mema”.. Ni ngumu kwa ibilisi kumwachisha mtu wa MUNGU mema!.. hawezi kumfundisha moja kwa moja aache mema, ni jambo gumu sana kwake, ingekuwa ngumu kwa shetani kumshawishi HAWA pale bustanini amwambudu yeye na aache kumwambudu MUNGU, Hawa asingeweza kumsikiliza nyoka)..ni jambo gumu sana.

Lakini adui alikuja na injili ya uvuguvugu, kwamba aendelee na mema, lakini na mabaya pia ayafanye kidogo na MUNGU atamkubali!.. kwaufupi afanye mema kidogo na mabaya kidogo, asiwe moto, awe vuguvugu kwani bado MUNGU atamkubali..pasipo kujua ni mtego mbaya, sana wa kutapikwa moja kwa moja na MUNGU.

Ufunuo 3:15 “Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.

16 Basi, KWA SABABU UNA UVUGUVUGU, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu”.

Ni jambo hilo hilo, analiendeleza leo katika kuwaangusha watu wa MUNGU waliosimama, anawashawishi kuamini kuwa Ukiwa mtu wa kiMungu sana utachanganyikiwa, ni lazima uchanganye na mambo mengine madogo madogo ya kiulimwengu..

Ijapokuwa umeshakuwa mkristo, unaenda kanisani, unatoa sadaka, basi siku moja moja onja mvinyo, ijapokuwa hutukani, huna ugomvi na mtu na unasaidia masikini sio mbaya pia siku mojamoja kwenda kwenye dansi za starehe, ijapokuwa huibi, hudhulumu sio mbaya ukifanya uasherati mara moja moja..Hii ni sumu hatari sana, iliyowaangusha wazazi wetu wa kwanza.

Jihadhari na roho ya uvuguvugu, kwani unamtoa mtu moja kwa moja kutoka katika Neema ya MUNGU.

Je umempokea YESU?. Unao uhakika wa uzima wa milele baada ya maisha haya?..Fahamu kuwa uzima wa milele upo kwa YESU tu, na si mwingine.

Yohana 17:3 “Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma”.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

KUJITAKASA NI MUHURI WA UTAKATIFU

MAANA HUYAWAZI YALIYO YA MUNGU, BALI YA WANADAMU

Biblia inamaana gani inaposema “Mungu wa neema yote” (1Petro 5:10)

Je Sulemani alifuga nyani? (2Nyakati 9:21)

MAISHA YA UVUGUVUGU, YANAMFANYA MUNGU AUMWE.

WhatsApp
DOWNLOAD PDF

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2026/04/27/epuka-uvuguvugu/