MTU WA NNE, ANADHIHIRISHWA KWA MOTO

by Nuru ya Upendo | 20 May 2026 08:46 pm05

Shedraki, Meshaki, na Abednego, walipokataa kuisujudia sanamu ya mfalme, kama tusomavyo maandiko, walifungwa na kutupwa kwenye tanuru ya moto,  lakini wakiwa kule motoni, alionekana mtu wa nne, ambaye mfalme Nebukadreza alimwona kama mwana wa Mungu,  ndiye Yesu Kristo mwenyewe.

Danieli 3:24  Ndipo Nebukadreza akastaajabu, akainuka kwa haraka; akanena, akawaambia mawaziri wake, Je! Hatukutupa watu watatu, hali wamefungwa, katikati ya moto? Wakajibu, wakamwambia mfalme, Kweli, Ee mfalme.
25 Akajibu, akasema, Tazama, mimi naona watu wanne, nao wamefunguliwa, wanatembea katikati ya moto hali hawana dhara; na sura yake yule wa nne ni mfano wa mwana wa miungu.

Nachotaka ufahamu ni kwamba mtu wa nne, alikuwa Pamoja nao, siku zote, lakini kufunuliwa machoni pa watu, ilihitaji moto, ikiwa na maana nje ya moto, hakutambulika Dhahiri machoni pa wengi, bali kwa wale tu waliomwamini, tena mioyoni mwao.

Moto ni nini?

Moto, ni shinikizo lolote juu ya Imani ya mtu kwa Yesu Kristo, ambalo wakati mwingine  linahatarisha hata maisha yake. Huu moto wengi wanaukwepo lakini hawajui kuwa ndio unaompa Kristo nafasi ya kujifunua zaidi kwenye maisha yako.

Ukiona unataka kufukuzwa kazi kisa, siku za jumapili huwendi kazini unahudhuria ibadani, fahamu kuwa Kristo anaumbika Dhahiri kwenye maisha yako.

Ukiona unahatarisha biashara yako, kisa umegoma kula rushwa, ndivyo Kristo anakwenda kuonekana Dhahiri kwenye kazi zako, ni jambo tu la muda..

Ukiona, unafukuzwa, unapigwa, unafungwa, kwasababu ya msimamo wako mkali wa kimafundisho unaokemea dhambi, ujue kuwa, Kristo anakwenda kusimama na wewe kwa viwango vingine vya juu sana.

Moto kimsingi si mzuri, upitapo ni lazima utasikia maumuvi, lakini mbele ya Kristo, hauna nguvu, hivyo vitisho, mapigo, vifungo, dhihaka, havina nguvu yoyote, kwasababu yeye yupo Pamoja na wewe muda huo, ndivyo ilivyokuwa kwa Shedraki, Meshaki na Abednego, hawakuungua kwasababu ya ule moto.

Badili fikra zako, badala ya kuhuzunika kwa majaribu, Bwana anasema furahi, kwasababu huko ndipo viwango vyetu vya kumuona Kristo vipo.

Maran atha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Kwanini Mungu azungumze na Ayubu kupitia upepo wa kisulisuli (Ayubu 38:1)

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 13 (Kitabu cha Hosea).

USIYAKUBALI MARADHI YA MISRI

WhatsApp
DOWNLOAD PDF

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2026/05/20/mtu-wa-nne-anadhihirishwa-kwa-moto/