UKIMBIE UHURU WA ULIMWENGU

by Nuru ya Upendo | 26 May 2026 08:46 pm05

Umewahi kujua tofauti ya makundi haya mawili ya MBWA?.

Kundi la kwanza Mbwa wanaotembea huru barabarani na kundi la pili ni wale Mbwa wanaofugwa majumbani?.

Utaona Mbwa wanaozurula mitaani bila makao rasmi, huwa hawana afya, wanadharaulika, na ijapokuwa wanao uhuru wa kwenda popote watakapo lakini lakini bado huwa hawana afya huwa ni wenye maradhi.

Utaona mbwa anayekatiza mitaani, ataona vyakula vingi vinapikwa, ataona minofu mingi ikitengenezwa na wanadamu, atasikia harufu ya kila aina ya chakula kizuri lakini hatakula?.

Lakini tukirudi kwa wale Mbwa wanaofugwa majumbani ni kinyume chake.

Wao wana afya kwasababu wanalishwa na wanaowafuga, pia ni jasiri kwasababu wanaaminiwa na wanaowafuga.

Hawana haja ya kuhangaika kutafuta chakula kwani wanaletewa, hawana haja ya kujitibu kwani wanatibiwa na wanaowafuga mwa ufupi wanaishi maisha ya raha isipikuwa tu hawana uhuru wa kuzurula ovyo na kukatiza mitaani.

Ni hivyo hivyo kwa watoto waliotoroka kwao na kuishi mitaani, huwa hawana afya njema, wala ustawi ijapokuwa wana uhuru wa kufika popote watakapo na kufanya chochote watakacho..

Lakini watoto wanaolelewa nyumbani hawana uhuru wa kwenda popote watakapo au kufanya chochote watakacho lakini ndio wenye ustawi mzuri na wanaofanikiwa.

Ni hivyo hivyo kwetu pia, Uhuru wa kufanya chochote na kutenda chochote tutakacho ni uhuru potofu ambao, mwisho wake ni kuharibika na kudharaulika.

Lakini tukikubali kulelewa na MUNGU kama watoto wanaopendwa basi tutafika mbali na kustawi sana.

Kama upo nje ya hifadhi rudi nyumbani kwa baba yako leo, kwa kutubu dhambi na kumkaribisha YESU, Na Bwana atakupokea na kukulea kama watoto anayependwa sana.

Waefeso 5:1 “Hivyo mfuateni Mungu, kama watoto wanaopendwa”.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

WhatsApp
DOWNLOAD PDF

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2026/05/26/ukimbie-uhuru-wa-ulimwengu/