LITUKUZE JINA LA BWANA

by Nuru ya Upendo | 8 June 2026 08:46 am06

Jina la Bwana YESU KRISTO libarikiwe daima.

Karibu tujifunze Biblia,

Je unajua ni kitu gani kilichotukuka sana kwa MUNGU?.

Hiko si kingine zaidi ya jina lake, tangu enzi MUNGU amekuwa akijitambulisha kwa JINA na si SURA.

Ndio maana katika ile sala ya Bwana, inaanza na “Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe”..ndipo maombi mengine yafuate (Mathayo 6:9).

Na hata Bwana wetu YESU aliomba hivyo..

Yohana 12:28 “Baba, ulitukuze jina lako. Basi ikaja sauti kutoka mbinguni, Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena”.

Na kila kitu tunafanya kwa jina la MUNGU na si kwa sura ya MUNGU. ( Wakolosai 3:17).

Kwahiyo jina ni kitu kilichotukuka sana, lakini sasa inapotokea jina la mtu au watu linapoinuliwa zaidi ya jina la MUNGU, ni jambo linaloleta Wivu mkubwa kwa MUNGU wetu soma (Kutoka 34:14).

Ndilo kosa walilolifanya watu wa Babeli..walipojenga mji na mnara ambao lengo lake ni kujijengea jina, na wala si kumjengea Bwana jina.

Mwanzo 11:4 “Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, TUJIFANYIE JINA; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote

15 BWANA akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu”.

Kama umempokea YESU yoyote uyafanyayo yafanye kwa utukufu wa jina la MUNGU na si wa jina lako.

Biashara yako iwe kwa utukufu wa jina la Bwana zaidi ya utukufu wako, watu wakiona kustawi kwako walitukuze jina la MUNGU wako na si jina lako.

Watu wakiona mwenendo wako jina la MUNGU wako litukuzwe na si litukanwe.

2 Wathesalonike 1:12 “jina la Bwana wetu Yesu litukuzwe ndani yenu, nanyi ndani yake, kwa neema ya Mungu wetu na ya Bwana Yesu Kristo”.

Tukienda kwa kanuni hiyo tutafanikiwa sana kiroho..

Maran atha.

 

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

WhatsApp
DOWNLOAD PDF

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2026/06/08/litukuze-jina-la-bwana/