by Nuru ya Upendo | 17 June 2026 08:46 am06
Swali: Ubatizo ni kitendo cha kuzama kwenye maji na kuibuka juu ambacho ni kiashirio cha kufa na kufufuka pamoja na YESU kiujumla ni kuwa Mpya, je mfano umeokoka halafu ukaenda mtoni peke yako kwa Imani ukazama wewe mwenyewe na kuibuka juu je ubatizo huo utakuwa batili?
Jibu: Tukirejea ubatizo wa Bwana YESU tunaona ilimpasa aende Yordani akabatizwe na Yohana, kulikuwa na uwezekano wa Bwana YESU kutokwenda kabisa kubatizwa na Yohana na akaenda mwenyewe majini.. lakini ilimpasa aende kwa lengo la kutufundisha sisi…
Mtu anapobatizwa ni ishara ya kuzaliwa (soma Yohana 3:3-5)
Yohana 3:3 “Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, MTU ASIPOZALIWA MARA YA PILI, HAWEZI KUUONA UFALME WA MUNGU.
4 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?
5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, MTU ASIPOZALIWA KWA MAJI NA KWA ROHO, HAWEZI KUUINGIA UFALME WA MUNGU”.
Sasa kwa kawaida “hakuna mtu anayeweza kujizaa mwenyewe”.. maana yake hakuna mtu asiye na baba au mama.. kila mtu ni lazima awe na wazazi wawe wema au wabaya.
Na kwa mantiki hiyo hiyo mtu anayejibatiza mwenyewe ni sawa na amejizaa mwenyewe, jambo ambalo haliwezekani.
Kwahiyo ni lazima mtu akabatizwe na mwingine aliyemtangulia kiimani, ambaye ndiye atakayesimama kama mzazi wake wa kiroho kwa wakati huo.. na si sahihi mtu kujibatiza mwenyewe na pia kwenye Biblia hapaoneshi mahali popote kuna mtu aliyejibatiza bali wote walibatizwa na wengine waliowatangulia kiimani, kuanzia Bwana wetu YESU KRISTO na mitume wote na watu wote (soma Yohana 3:13-17, Matendo 9:17-18, Matendo 8:12-14, Matendo 19:1-5).
Na Bwana mwenyewe pia alitoa agizo kwa mitume kwamba wakawabatize watu na si watu wakajibatize wenyewe (Mathayo 28:19).
Kwahiyo kwa hitimisho si sahihi kujibatiza, na pia ubatizo ni lazima kwa kila mwamini, na ni lazima uwe ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Bwana YESU KRISTO (Matendo 2:38)
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2026/06/17/je-mtu-anaweza-kujibatiza-mwenyewe-mtoni/
Copyright ©2026 Wingu la Mashahidi unless otherwise noted.