by Nuru ya Upendo | 17 June 2026 08:46 pm06
Chanzo kibaya, Haimaanishi mwisho mbovu, chanzo chaweza kuwa bora lakini mwisho ukawa mbovu, Vilevile chanzo chaweza kuwa kibovu, mwisho ukawa mzuri.
Moja kati ya watu waliofanya uasi mkubwa mpaka Mungu akawaangamiza kwa kuwashusha kuzimu moja kwa moja wakiwa wazima, basi alikuwa ni Kora na jamii ya watu wake.
Ni mtu ambaye anatajwa hata baadaye katika agano jipya (Yuda:1:11), kama kielelezo akifananishwa na watu waasi waliopotoka wa siku za mwisho, kwasababu ya maasi yake kuwa makubwa yenye kuambukiza.
Hesabu 16:31-33
[31]Basi ilikuwa, hapo alipokwisha kusema maneno haya yote, nchi iliyokuwa chini yao ikapasuka;
[32]nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza, na watu wa nyumba zao na wote walioshikamana na Kora, na vyombo vyao vyote.
[33]Basi wao, na wote waliokuwa nao, wakashukia shimoni wali hai; nayo nchi ikawafunika wakaangamia kutoka mle mkutanoni.
Lakini ijapokuwa wazazi walifanya vibaya…watoto hawakufuata njia za baba yao (Hesabu 26:11)
Kinyume chake baadaye tunaona wazao wa kora wakaambata na Bwana kwa bidii mpaka wakawa sehemu takatifu ya Mungu, yaani waimbaji wa hekaluni.
Nafasi iliyo takatifu sana.
1 Nyakati 6:31–38,
Wengine wakawa wafungua malango ya nyumba ya Mungu (1 Nyakati 9:19)
Na Kama hilo halitoshi Sehemu nyingi za Zaburi zilitungwa na wana wa Kora. Mfano wa hizo ni
(Zaburi 42, 44, 45, 46, 47, 48, 49, 84, 85, 87, 88).
Huu ni mchango mkubwa sana kwenye ufalme wa Mungu. Ambao mpaka sasa tunakula matunda yake.
Lakini si rahisi kukubali kama hao ni wana wa mtu mwasi Kora. Ni sawa na leo usikie wana wa Yezebeli ni manabii wa Bwana.., wana wa Elima-mchawi ni mitume wa Kristo.
Tufahamu kuwa rehema za Mungu, haziathiriwi na asili, au mwanzo mbovu. Maadamu moyo umegeuka kweli kweli, Bwana huanza historia mpya.
Hapo mwanzo uliitwa Kora lakini leo ukigeuka utaitwa Musa, uliitwa Sauli leo utaitwa Paulo.
Sahau yaliyopita, anza ukurasa mpya na Bwana. Wazazi wako walikosea, hata na wewe mwenyewe ukakosea, ukapata sifa mbaya, ukawa kama mfu, . LEO HII, kubali toba ya kweli, uwe kiumbe kipya, ukubaliwe na Bwana, upendwe na Bwana, utumiwe na Bwana, hata kama una asili ya sifa mbaya.
Je upo tayari leo kukata shauri kwa kutubu na kumpokea Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yako?
Kama ndio basi hapo ulipo piga magoti kisha sema sala hii kwa imani kutoka moyoni ukimaanisha kabisa kutaka ukombozi wa nafsi yako leo. SEMA;
“Bwana Yesu, asante kwa upendo wako mkuu, kwa kuja duniani kunikomboka maisha yangu, katika dhambi na hukumu. Leo hii nimeamini kwa moyo wangu wote, na kupokea msamaha wa dhambi upatikanao kwa dhabihu ya damu yako takatifu. Kuanzia leo mimi ni mwana wa Mungu, nimemkataa shetani na kazi zake zote. Karibu Roho Mtakatifu ndani yangu. Ufanye makao yako sasa, nitembee kwa nguvu zako, na kukutumikia. Nimeomba nikiamini katika jina la Yesu Kristo.
Amen
Mpaka hapo utakuwa umepokea msamaha wa dhambi, hivyo hatua zinazofuata na malezi ya kiroho ili umjue Mungu, ukue kiroho, Na ubatizo ikiwa bado hujabatizwa.
Kwa mawasiliano.
Piga namba hizi : +255789001312 / +255693036618
Lakini tembelea tovuti yetu yenye mafundisho mengi zaidi ya elfu tano (5000), upate kujifunza kufuatana na mada mbalimbali za kiroho.
Mungu akubariki.
ashirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2026/06/17/kora-na-watoto-wake/
Copyright ©2026 Wingu la Mashahidi unless otherwise noted.