UPANGA USHIKAMANAO NA MKONO

by Nuru ya Upendo | 7 July 2026 08:46 pm07

2 Samweli 23:9-10

[9]Na baada yake kulikuwa na Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale mashujaa watatu waliokuwa pamoja na Daudi; walipowatukana Wafilisti waliokuwa wamekusanyika huko ili kupigana, na watu wa Israeli walikuwa wamekwenda zao; 

[10]huyo aliinuka, akawapiga Wafilisti hata mkono wake ukachoka, na mkono wake ukaambatana na upanga; naye BWANA akafanya wokovu mkuu siku ile; nao watu wakarudi nyuma yake ili kuteka nyara tu. 

Kibaolojia mwili wa mwanadamu unapokamata kitu, kwa muda mrefu sana, kwa nguvu, huwa unatabia ya kukakamaa katika hali hiyo hiyo hata kama mtu huyo hatakuwa na nia ya kuendelea kukishikilia kitu hicho.

Ndicho kilichomkuta huyu shujaa wa Daudi, alipokutana na jeshi la wafilisti angali yupo peke yake. Aligundua kitu pekee ambacho kingeweza kumtetea ni upanga wake. Hivyo aliukamata kwa nguvu sana bila kuuachia, akaanza kupambana na wafilisti wale kwa muda mrefu,  hakujua kuwa mkono wake utabakia katika hali ile ile…yeye aliendelea tu kupigana vita, mpaka  baadaye aliposhangaa  kuona hana jitihada yoyote tena ya kuushika upanga, ni kama vile ulikuwa ni sehemu ya kiungo chake…kazi yale ilikuwa ni kurusha tu mkono kuupeleka anapotaka, huku upanga ukiwa tu pale pale kiganjani hautoki…

Kikawaida hali ikishafikia hatua hiyo huwa inamgharimu mtu masaa mengi hata siku,  ili kung’atuka kutoka kwenye kitu kilichoshikamana naye..wakati mwingine ili kuharakisha uponyaji, wengine hutumia maji ya uvuguvugu na kuchua kiganja kwa muda baadaye kunyosha kidole kimoja baada ya kingine…

Sasa askari wa mwilini ni kivuli cha mtu wa rohoni. Yeye naye ana mikono na analazimika wakati wote kuwa na upanga…Lakini si upanga tu, wa kushika, bali ule Ugandao na mkono. 

Waefeso 6:11-14,17

[11]Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. 

[12]Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 

[13]Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. 

[14]Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,..

[17]Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; 

Kama maandiko yanavyotuonyesha hapo Mtu wa rohoni, hulazimika kubeba upanga wake, ambao ni Neno la Mungu.

Tunapoonyesha nia ya kuling’ang’ania Neno la Mungu, mwanzoni ni kama tutatumia jitihada zetu, lakini haitakuwa hivyo mbeleni …baadaye litashikamana na sisi..maana yake haitakuwa jitihada tena kuliishi.

Jambo lolote la kiroho, mfano maombi ya masafa marefu, mwanzoni ukianza utaona kama ni jitihada zinatumika lakini ukiendelea mara mbili, mara tatu utaona ni kawaida..

Mambo yote ya rohoni iwe ni upendo, unyenyekevu, utaanza kwa jitihada fulani lakini Kwasababu umekusudia tu kung’ang’nia kwa nguvu, utagandamana navyo.

Kumbuka hakuna wepesi wowote utakuja bila mtu kutia nia kwanza. Anza sasa kutendea kazi Neno la Mungu.

Bwana akubariki.

 

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:


 

WhatsApp
DOWNLOAD PDF

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2026/07/07/upanga-ushikamanao-na-mkono/