by Nuru ya Upendo | 9 July 2026 08:46 am07
Biblia inatuonyesha Mungu ndiye muumba wa vitu vyote
Mwanzo 1:1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.
Lakini hatujui ni nini kilitokea baadaye kikaifanya dunia kuwa ukiwa, mpaka akaanza kuirekebisha tena dunia aliyoiumba mwanzo..
Kwasababu mstari wa 2..unasema nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji,
Mungu akaanza tena kuifanya ikaliwe na watu, akaleta tena nuru kutoka kwenye giza, akayatenga maji, na kuyaweka sehemu stahiki, akalitokeza anga..akamuumba mwanadamu.
Dunia ikawa nzuri tena, lakini baadaye mwanadamu akaasi, akaiharibu duniani, mpaka ikaangamia kwa maji.
Bado Mungu hakuikatia tamaa dunia yake, akawaongeza,Nuhu na wazao wake, baadaye akamchagua Ibrahimu ili kumwandaa mkombozi atakayeikomboa dunia kikamilifu, akaja Kristo ulimwenguni ndio mwokozi wetu.
Watu wakaokolewa, ijapokuwa waliendelea kuiharibu dunia, bado Mungu akawa kwenye mwendelezo wa uumbaji wake unaoharibiwa .
Na kama tunavyojua Kristo aliahidi kurudi tena duniani mara ya pili, kuwanyakua watu wake, kisha kuukarabati huu ulimwenguni na kuufanya kuwa mbingu mpya na nchi mpya.(Ufunuo 21)
Hivyo kama ukichunguza asili ya tabia ya Mungu, si kufanya kitu mara moja, kisha pale kinapoharibika anakikatia tamaa ..
Hapana utaona hukiumba tena na tena na tena…kwa miaka na miaka na miaka..tena huanzia mbali sana mpango wake wa ukarabati..
Na sisi ni lazima tujue tumeumbwa kwa mfano wake na sura yake..ikiwa unaona hakuna mwenye hekima duniani kumzidi Mungu, na kila lifanyalo ni bora, na kamilifu basi jifunze kuiga tabia zake ufanikiwe…
Mungu wetu alikuwa na siku moja katika juma ya kupumzika, wewe si ‘busy’ zaidi ya Mungu mpaka siku zote saba katika juma, mwaka mzima unafanya kazi mpaka unakosa muda wa kumwabudu Mungu wako.
Vivyo hivyo ni lazima kutambua kuwa kazi zake zimepitia changamoto nyingi sana za kuharibiwa zaidi ya zako lakini amekuwa katika uumbaji wake kila siku..Na wewe pia kuharibiwa kwa maono yako, si sababu ya kukata tamaa na kusema sitaendelea mbele…inuka anza tena na tena..
Unamtumikia Mungu, ile huduma iliyokaa ndani yako, ni kama imekufa, mwanzoni uliona hatua lakini sasa huoni, pengine ni kutokana na kuwa umedhulumiwa, umeibiwa, umefukuzwa..inuka tena na tena, anza upya..
Kuacha kazi uliyokwisha itaabikia na kuitolea jasho jingi, ni ishara ya kuwa bado tabia ya Mungu haijaumbika ndani yako.
Kumbuka mpaka leo hii Mungu anaendelea kufanya uumbaji wake, itapokuwa kazi hizo zingepeswa zikamilike tangu kule mwanzo…Wewe ni nani usifanye matengenezo yako yaliyokufa kila siku?
Anza sasa. Fanya kazi na Mungu.
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
MBONA MMESIMAMA HAPA MCHANA KUTWA BILA KAZI?
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2026/07/09/mungu-aumbaye-tena/
Copyright ©2026 Wingu la Mashahidi unless otherwise noted.