by Nuru ya Upendo | 20 July 2026 08:46 pm07
Jina la Bwana YESU libarikiwe, karibu tujifunze Biblia, Neno la Mungu wetu, lililo taa na Mwanga wa njia yetu.
Utatamani kutembea na wenye vyeo vikubwa vya ulimwengu, ambao wengi wa hao ni wafu kiroho,
Utatamani kuolewa na wenye mali nyingi, na uwezo mkubwa ambao wengi wa hao ni wafu rohoni.
Utawadharau wanaoonekana dhaifu na wanyonge ambao Biblia inawataja kama matajiri wa imani na walio hai kiroho..
Yakobo 2:5 “Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?”
Dada ni heri uambatane na huyo mtu ambaye unamwona leo ni maskini lakini anaye YESU, kuliko uende kuolewa na tajiri ambaye hana YESU maishani ( ni mfu kiroho).
Heri uwe na marafiki maskini lakini wanaye YESU kuliko uwe na marafiki matajiri ambao ndani yao hawana uzima.
Huyo tajiri kwako ni “Simba” na huyo maskini kwako ni “Mbwa”…ambaye ni kama hana hadhi mbele ya macho yako lakini Biblia inatufundisha kinyume na hilo..
Mhubiri 9:4 “Kwa kuwa liko tumaini kwa yule aliyeambatana na wote walio hai; (maana ni afadhali mbwa aliye hai kuliko simba aliyekufa)”.
Ni afadhali mbwa, anayeishi, maana yake ni heri mtu maskini na mdhaifu mwenye uhai wa rohoni kuliko mtu aliye simba (yaani mwenye nguvu na mkali) lakini ni mfu rohoni.
Chagua kwa makini nani wa kuambatana naye..
2 Wakorintho 6:14 “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?
15 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari?Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?”
Bwana atusaidie..
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2026/07/20/ambatana-na-wali-hai-rohoni/
Copyright ©2026 Wingu la Mashahidi unless otherwise noted.