ATAWAFANYIA WAMCHAO MATAKWA YAO.

by Nuru ya Upendo | 22 July 2026 08:46 am07

Zaburi 145:19 “Atawafanyia wamchao matakwa yao, Naye atakisikia kilio chao na kuwaokoa”.

Pamoja na kwamba tumeagizwa kuomba “Mapenzi yake yatimie/yatimizwe (Mathayo 6:10”.

Lakini “Siri” moja kuu ni kwamba zaidi ya asilimia 90 ya Maombi ya wanaomcha MUNGU ni mapenzi ya MUNGU.Kwanini?..

Kwasababu maandiko yanatuambia hapo kuwa “Atawafanyia wamchao matakwa yao, Naye atakisikia kilio chao na kuwaokoa”.

Zingatia hilo neno “Atawafanyia wamchao matakwa yao”.

Kumbe Mungu anawapatia watu wake wanaomcha “Matakwa yao, yaani haja zao wanazozitaka”.

Kwa mtu anayemcha Mungu akiomba amani, ni asilimia kubwa ya hitaji lake hilo kuwa ni mapenzi ya MUNGU.

Mtu anayemcha MUNGU akiomba afya, ni asilimia zaidi ya nusu kuwa anaomba jambo ambalo ni mapenzi ya MUNGU.

Mtu anayemcha MUNGU akiomba akiomba mambo mengine yote ikiwemo mafanikio ya kiroho na kimwili ni mapenzi ya MUNGU, kwasababu MUNGU anawapa wamchao matakwa yao.

Je unataka kupewa matakwa yako na MUNGU?.Jibu ni rahisi “Mche Mungu tu”..Na Biblia inasema kumcha Mungu ndio hekima na kuepukana na uovu ndio ufahamu (Ayubu 28:28).

Sasa hatuwezi kumcha MUNGU kwa nguvu zetu, inahitajika kuwezeshwa na Roho Mtakatifu, kwasababu tabia ya kumcha MUNGU, ni zao la Roho Mtakatifu.Isaya 11:2 “Na roho ya BWANA atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, ROHO YA MAARIFA NA YA KUMCHA BWANA”.

Sasa kama kumcha Bwana ni zao la Roho Mtakatifu, je tunampataje Roho Mtakatifu..

Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?

38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”

Kumbe kanuni ya kupokea Roho ni kutubu na kubatizwa kwa jina la YESU KRISTO!.

Basi maana yake tukitubu na kubatizwa tutapokea Roho Mtakatifu kama ilivyoandikwa, na matokeo ya kujaa Roho Mtakatifu, ni uwezo wa kumcha MUNGU kuingia ndani yako.Na matokeo ya kumcha MUNGU sana ni kusikiwa maombi yako na Bwana kukupa matakwa yako.

Je umeokoka?..Je unamcha Bwana?.

Zaburi 112:1 “Haleluya. Heri mtu yule amchaye BWANA, Apendezwaye sana na maagizo yake.

2 Wazao wake watakuwa hodari duniani; Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa”.

3 Nyumbani mwake mna utajiri na mali, Na haki yake yakaa milele”.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

WhatsApp
DOWNLOAD PDF

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2026/07/22/atawafanyia-wamchao-matakwa-yao/