Category Archive home1

UFAHAMU UFUNGUO WA KUMPENDA BWANA ZAIDI

Je unaujua ufunguo wa wewe kumpenda Bwana zaidi?.. kuna jambo ukilifanya basi upendo wako kwa MUNGU utaongezeka kwa kiwango kikubwa sana.. Utajikuta unampenda MUNGU zaidi, unamheshimu zaidi na unamtumikia zaidi.

Na ufunguo huo si mwingine zaidi ya kuutafakari MSAMAHA WAKE KWAKO KWA MAPANA!.. Unaweza kuona jambo la msahama kwako ni dogo tu!.. Lakini nataka nikuambie Msamaha wa MUNGU kwako una uhusiano mkubwa sana na UPENDO WAKO KWAKE!.

Maandiko yanasema “aliyesamehewa sana hupenda sana, na aliyesamehewa kidogo hupenda kidogo”

Luka 7:47 “Kwa ajili ya hayo nakuambia, Amesamehewa dhambi zake ambazo ni nyingi kwa kuwa amependa sana; lakini asamehewaye kidogo, huyo hupenda kidogo”.

Hebu tafakari huu mfano: Mtu mmoja alikuwa anadaiwa shilingi 500 na mwenzake na akasamehewa na mwingine aliukwa anadaiwa shilingi laki 5 na mtu huyo huyo mmoja, naye pia akasamehewa kiasi chote cha pesa (shilingi laki 5)..

Je yupi kati ya hao wadaiwa wawili waliosamehewa, atampenda zaidi Yule aliyewasamehe?.. Bila shaka Yule aliyesamehewa deni kubwa ndiye atakayempenda zaidi aliyemsamehe, na hata kumheshimu sana..

Lakini Yule aliyesamehewa deni dogo, anaweza kuwa mtu wa shukrani lakini si katika kiwango kikubwa, na wala hawezi kutoa heshima ya kiwango kikubwa kwa yule aliyemsamehe.

Ni hivyo hivyo katika upande wa Imani, watu waliojiona ni wenye dhambi nyingi na kubwa kubwa!, na kujiona kama hawajastahili msahama kwa makosa yao, wanapoungama na kupokea msamaha, huwa wanampenda sana Bwana YESU na kumheshimu.

Lakini watu wanaojiona ni wasafi au watakatifu sana, kwamba hawamkosei sana MUNGU huwa hata upendo na MUNGU hawana, au upo kwa kiwango kidogo.

Sasa kiuhalisia wote tumemkosea MUNGU pakubwa sana!.. ukijiona huna dhambi nyingi, basi fahamu kuwa kuna shida kwako ya kutafakari, ambayo hiyo sasa ndio unapaswa ushughulike nayo.

Unapaswa ushughulike na hiyo hali mpaka ifikie hatua ujijue kuwa hukustahili, na wewe ulikuwa ni mbaya mno, na mbovu, na makosa yako yalikuwa makubwa sana!.. ukiweza kufikia hiyo tafakari, basi jua matunda yako ni wewe kumpenda BWANA na kumheshimu sana.

Unawezekana wewe sio mwizi, au muuaji au mzinzi lakini hebu tafakari vipindi ulivyomsema ndugu yako, na MUNGU alikufumbia macho, ingawa ulistahili adhabu ya mauti papo kwa hapo.

Hebu tafakari vipindi ulivyotamani vitu visivyofaa moyoni mwako, na MUNGU alikufumbia macho ingawa ulistahili kufa papo kwa hapo.

Hebu tafakari vipindi ulivyokasirika bila sababu, tafakari vipindi uliyokuwa unawaza mawazo mabaya, tafakari vipindi ulivyodanganya na kusema uongo, tafakari vipindi miguu yako ilipokuwa inaelekea kufanya maovu, tufakari vipindi ulivyotukana mdomoni na moyoni mwako, tafakari mambo ya upumbavu uliyoyafanya mitandaoni,  hayo yote si kwamba MUNGU alikuwa haoni, au hata sasa hayaoni, anayaona yote!.

Inawezekana hujawahi kuua, lakini tafakari vipindi ulivyokuwa mbinafsi, tafakari visasi na vinyongo ulivyokuwa navyo, na huenda unavyo hata sasa, tafakari udunia wote ulioufanya, rudi nyuma kumbuka tukio moja baada ya lingine katika maisha yako, yatakafari sana halafu fikiri YESU AMEJITWIKA makosa yako yote hayo, ambayo kama si rehema zake huenda ungekuwa umeshakufa na upo KUZIMU sasa!.

Lakini alikizuia kifo kisikupate!, umempa nini?, au una umaalumu gani hata akusamehe hayo yote?, kwani waliokufa bila kupata huu msamaha wana kasoro gani zaidi yako?.

Je huoni kama aliyekupa huu msahama ni wa thamani kubwa? Huoni kama amekusamehe makubwa sana.. bado humpendi tu!.. ungepaswa uwe kuzimu muda huu, lakini bado unaishi! Bado kwako unamwona vile vile?

Ndugu tenga muda sana utafakari msamaha wa YESU, kwani ndio uliobeba funguo za kumpenda YESU zaidi, Ukiutafakari msamaha wa YESU utaishia kumpenda, lakini pia kumwogopa (kutokutenda dhambi tena)

Zaburi 130:4 “Bwana, kama Wewe ungehesabu maovu, Ee Bwana, nani angesimama?

4 Lakini kwako kuna msamaha, Ili Wewe uogopwe”.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NGUVU YA MSAMAHA

UMUHIMU WA KUOMBA MSAMAHA.

NI KWA NAMNA GANI KRISTO ALIZIBEBA DHAMBI ZETU?

JE UMEUPOKEA UWEZA WOTE WA UUNGU NDANI YAKO?

Hadhari ni nini kibiblia? (Mithali 1:4)

Print this post

Yesu aitwaye Yusto alikuwa ni nani? (Wakolosai 4:11).

Swali: Je huyu Yesu anayetwaja katika Wakolosia 4:11 alikuwa ni nani, na je ni kwanini aitwe hilo jina tukufu?


Jibu: Turejee..

Wakolosai 4:11 “Na YESU AITWAYE YUSTO; hao ni watu wa tohara. Tena hao peke yao ni watendaji wa kazi pamoja nami kwa ajili ya ufalme wa Mungu; nao walikuwa faraja kwangu”.

Katika Biblia Kristo mwokozi wetu hakuwa wa kwanza kuitwa jina YESU, bali walikuwepo watu wengine kadhaa kabla yake walioitwa kwa hilo jina, kwani lilikuwa ni jina linalojulikana Israeli yote,

Na tafsiri ya jina YESU ni  (YEHOVA-MWOKOZI), kama vile ilivyokuwepo YEHOVA-YIRE ambayo tafsiri yake ni YEHOVA mpaji n.k

Kwahiyo YESU ni jina lililokuwepo hapo kabla, kama tu Simeoni aliyeitwa Petro, hakuwa wa kwanza kuitwa Simeoni, au Yuda aliyemsaliti Bwana YESU hakuwa wa kwanza kuitwa Yuda, kwani hata mtoto wa Yakobo,  aliitwa Yuda, na ndio ukoo Bwana YESU aliotokea.

Sasa ni kitu gani kilichomtofuatisha YESU mwokozi wetu na maYesu wengine?.. si kitu kingine bali ni kiunganishi cha mwisho cha jina hilo,.. Aliyetufia anajulikana kama YESU KRISTO,  maana yake YESU MTIWA MAFUTA na MUNGU…

Wengine wanaitwa “Yesu wa Yusto”, wengine “Bar-YESU” (soma Matendo 13:6) lakini ni mmoja tu anaitwa “YESU KRISTO”.. Huyu kwa jina lake hili ndio tunapata ondoleo la dhambi na wokovu (Matendo 4:12).

Na kwa jina la YESU KRISTO, Tunafunguliwa na kuponywa magonjwa yetu, na ziadi sana ndio kwa jina hili tunapaswa tuhubiri na kuhubiriwa ili tupate ukombozi.

Lakini katika hizi siku za mwisho shetani amewanyanyua maYesu wengi wa uongo, ambao na si Yule wa uzima.

2Wakorintho 11:3 “Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.

4 MAANA YEYE AJAYE AKIHUBIRI YESU MWINGINE AMBAYE SISI HATUKUMHUBIRI, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana naye!”

Yesu mwingine, (asiye KRISTO) anahubiriwa sasa na manabii na watumishi wa uongo, ambaye yeye hahitaji utakatifu.. ukiona unahubiriwa kwa jina la YESU lakini injili hiyo haikupeleki kuwa msafi mwilini na rohoni, badala yake unazidi kuwa wa kidunia, fikiri mara mbili ni Yesu gani uliyempokea, kwahiyo hatuna budi kujipima.

Lakini tukirudi kwenye swali!, Je huyu Yesu aitwaye Yusto alikuwa ni nani?..

Huyu Yesu aitwaye Yusto, alikuwa ni mmoja wa wafuasi wa Bwana wetu YESU KRISTO, ambaye alishirikiana na akina Paulo (watumishi wa MUNGU) kuhubiri injili, na alikuwa ni Myahudi (ndio maana Biblia inasema hapo alikuwa ni mtu wa tohara, maana yake aliyetahiriwa).

Maana ya jina Yusto ni “mwenye haki”.. na aliitwa “Yesu aitwaye Yusto”, kumtofautisha na YESU KRISTO. Huyu hakusimama kutaka aabudiwe, bali kinyume chake alikuwa anamhubiri YESU KRISTO.

Je umempokea Bwana YESU KRISTO?. Kama bado unasubiri nini?

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

JE BWANA YESU ALIMTOKEA YUDA BAADA YA KUFUFUKA KWAKE?.

MANENO SABA YA YESU MSALABANI.

YESU MNAZARETI,  ANWANI YA MSALABA.

Je shetani ana uwezo wa kujua mawazo ya mtu?

Uchambuzi na mwandishi wa kitabu cha Waefeso.

Print this post