Kuhusu sisi

by Admin | 4 Oktoba 2020 08:46 um10

wingu la mashahidi Wingu la Mashahidi  ni huduma isiyofungamana na dhehebu lolote. Wala haipo kwa lengo la kutangaza dhehebu la aina yoyote,

Lengo la huduma hii, ni kutangaza habari njema za wokovu ulioletwa na Bwana wetu Yesu Kristo, kwa njia mbalimbali hususani mitandaoni.

Tunaamini kuwa biblia ndio kitabu pekee kilichovuviwa na Roho Mtakatifu kwa lengo la kuwakomboa na kuwakamilisha wanadamu. Hivyo hicho ndio kitovu cha mafundisho yote yapatikanayo katika tovuti hii.

Tunaamini kuwa wokovu unatoka kwa mtu mmoja tu naye ni YESU KRISTO, Na huo unapatakana kwa kumwamini, kisha kubatizwa kwa jina lake, na kisha kupokea Roho Mtakatifu sawasawa na  Matendo 2:38

Tunaamini kuwa kanisa tunaloishi ndio kanisa la mwisho, lijulikanalo kama Laodikia (Ufunuo 3:14-22). Na kwamba hili ndio kanisa tutakaloshuhudia tukio la unyakuo.

Kumbuka: Wingu la Mashahidi wa Kristo Sio dhehebu la “Mashahidi wa Yehova”. bali jina hili limetoka katika kitabu cha Waebrania 12:1

 Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,

Hivyo mimi na wewe pia tunaweza tukawa sehemu ya wingu hilo la mashahidi wa Bwana wetu Yesu Kristo, kama walivyokuwa wale wa wakati ule. Na ndio lengo la tovuti hii, kuwakaribisha watu wote waliookoka kutoka katika pande zote za ulimwengu kushirikiana nasi katika kuipeleka injili ya Bwana wetu Yesu kwa watu wote.

Hivyo uwe huru kuwasiliana nasi, kwa kile kilicho ndani yako.

Na Bwana akubariki sana.

WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/kuhusu-sisi/