MPINGA-KRISTO

by Admin | 17 July 2018 08:46 am07

Mpinga-Kristo ni nani?

Vita kubwa inayoendelea duniani leo ni vita kati ya MUNGU na SHETANI. Mungu anatafuta roho za watu vile vile shetani naye anawinda roho za watu. Hizi roho mbili zimekuwa zikipingana siku zote tangu ulimwengu ulipoanza kukaliwa na wanadamu.

Lakini baada ya mwanadamu kuanguka Mungu alitumia njia zote kwa Roho wake kumvuta kwake tena, mwishoni akaona vema kumleta mwanawe mpendwa YESU KRISTO kwa dhumuni moja tu! kutupatanisha sisi na Mungu, ili katika yeye sisi sote tuokolewe.

Vivyo hivyo shetani naye, kwa kuona hivyo kwa roho yake ya uovu, alitumia njia zake zote za kuweza kumtoa mwanadamu katika kusudi la Mungu na kumvuta kwake, jambo hili lilianza tangu Edeni, tunaona shetani jinsi alivyomtumia Nyoka kumdanganya Hawa ili aipate roho yake. Hivyo basi ulipofika wakati alipoona Mungu amemleta mwokozi katika mwili yaani YESU KRISTO na kuwavuta wengi kwa BABA, yeye naye alianza mipango ya kumwandaa mtu mmoja ambaye atakuwa na kazi maalumu ya kuwavuta watu kwake na kwenda kinyume na huyo mmoja Mungu aliyemteua (yaani YESU KRISTO). Sasa mwana huyu wa shetani ndiye anayeitwa MPINGA-KRISTO.

Kumbuka vita vya kwanza kabla ya Kristo kuja vilikuwa ni roho kwa roho (yaani Roho wa Mungu dhidi ya roho ya shetani), lakini vita vya mwisho ni MTU dhidi ya MTU (yaani YESU KRISTO dhidi ya MPINGA-KRISTO).

Wakristo wengi wanapokosa shabaha ni pale wanaposhindwa kumfahamu YESU KRISTO ni nani na MPINGA-KRISTO ni nani?. Ukishindwa kumfahamu YESU KRISTO ni nani huwezi kumfahamu MPINGA-KRISTO ni nani.

Hawa wote wawili waliandikwa kwenye NENO la Mungu katika “SIRI”. Ikiwa na maana utendaji kazi wao ulihitaji “UFUNUO wa ROHO” Kuutambua. Embu kwa ufupi, tutazame siri iliyopo kwa YESU KRISTO ambayo ilikuwa imefichika kwa Muda mrefu na hata sasa baadhi ya watu bado imefichika machoni pao.

SIRI YA YESU KRISTO:

1 Timotheo 3:16 ” Na bila shaka SIRI YA UTAUWA NI KUU. Mungu alidhihirishwa katika MWILI, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.”

Ukisoma hapo utaona kuwa jambo hili Mungu aliliweka liwe SIRI,na sio kitu cha wazi ya kwamba Yesu Kristo alikuwa ni MUNGU KATIKA MWILI. Yaani ni Roho ya Mungu ikitenda kazi katika mwili, lakini wengi hawakulijua hilo walimkataa na kumsulubisha,na hata leo wengi hawalifahamu hilo. maana Bwana Yesu alisema “Yohana 5:43  Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo. “ unaona huyo mwingine BWANA YESU aliyemzungumzia akija kwa jina lake mtampokea ni MPINGA-KRISTO mwenyewe..tusome tena mstari ufuatao

1 Wakoritho 2:6-8″  Walakini iko HEKIMA tusemayo KATI YA WAKAMILIFU; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilika;

7 bali twanena HEKIMA YA MUNGU KATIKA SIRI, ILE HEKIMA ILIYOFICHWA, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu;

8 ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, WASINGALIMSULIBISHA BWANA WA UTUKUFU; “.

Kwa maandiko hayo hapo juu, hata leo watu katika mioyo yao wanamchukulia YESU KRISTO kama ni mtu wa kawaida kama walivyofanya watu wa kipindi kile, wanayadharau maneno yake sio kwa mdomo bali kwa matendo, lakini hawajui kuwa wanamkataa na kumsulibisha Mungu mwenyewe ambaye ni BWANA WA UTUKUFU,  kwa heshima aliitoa damu yake, imwagike kwa ajili ya dhambi zetu kutupatanisha sisi na yeye lakini bado leo hii unaichezea hii damu ya thamani, itafika wakati hii neema haitakuwepo tena.

SIRI YA MPINGA-KRISTO:

2 Wathesalonike 2:3 “Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; AKAFUNULIWA YULE MTU WA KUASI , MWANA WA UHARIBIFU;

4 YULE MPINGAMIZI, AJIINUAYE NAFSI YAKE JUU YA KILA KIITWACHO MUNGU AMA KUABUDIWA; hata yeye mwenyewe kuketi katika HEKALU LA MUNGU, AKIJIONYESHA NAFSI YAKE KANA KWAMBA YEYE NDIYE MUNGU.

5 Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo?

6 Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake.

7 Maana “ILE SIRI YA KUASI” HIVI SASA INATENDA KAZI; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.

8 Hapo ndipo atakapofunuliwa yule ASI, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake;

9 yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo;

10 na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.”

Ukisoma habari hiyo mstari wa saba inazungumzia SIRI YA KUASI ambayo inatenda kazi duniani, na hii siri ya kuasi inatenda kazi ndani ya yule ASI (ambaye ndio mpinga-kristo mwenyewe) kama maandiko yanavyomtaja kwenye mstari wa 9, kuwa “kutenda kwake kazi ni mfano wa kutenda kwake shetani mwenyewe”. Kama tu vile SIRI YA UTAUWA ilivyokuwa inatenda kazi ndani ya YESU KRISTO, na kutenda kwake kazi Yesu kulikuwa ni mfano wa kutenda kwake Mungu mwenyewe vivyo hivyo na huyu (Mpinga-kristo) siri ya kuasi inatenda kazi ndani yake na  kutenda kwake kazi kutakuwa ni mfano wa shetani.

JE HUYU MPINGA-KRISTO NI NANI?

Baada ya shetani kuona kuwa hawezi kuwapata wanadamu wengi kwa kutaka wamwabudu moja kwa moja kama wanadamu wamwabuduvyo Mungu, aliamua kujibadilisha na kujifanya kuwa kama malaika wa Nuru (2Wakoritho 11:14), ili awapate wale wanaoonyesha dalili ya kuipenda Nuru. Kumbuka shetani hafanyi vita na watu wa ulimwengu huu, kwasababu hao alishawapata na siku zote wapo gizani, kwahiyo ili awapate wale wa nuruni ni lazima ajigeuze kuwa mfano wa malaika wa Nuru, vivyo hivyo na watumishi wake nao ni lazima wajigeuze kuwa kama watumishi wa nuru. Hapo ndipo penye vita vikali pale mbwa-mwitu anapokuja kwa vazi la kondoo. Hivyo inahitaji hekima ya Roho Mtakatifu kumtambua mpinga-kristo vinginevyo hawatakaa ufahamu adui yako yupo wapi na anatendaje kazi.

Ndugu kuna vikundi vingi vya kishetani na kichawi, vinavyosifika kama freemason, rotary clubs, iluminati, ku klux klan, brotherhood, n.k. vimekuwa vikiogopeka kana kwamba hivyo ndio makao makuu ya shetani, usidanganyike vikundi hivyo shetani anavitumia kuwadaka watu wasiokuwa wakristo na wakristo wachache wenye imani isiyothabiti kwasababu mkristo wa kweli yoyote hawezi kwenda kwa mganga na shetani analijua hilo, wala hawezi kujiunga kwenye mojawapo ya hivyo vikundi wala kupiga ramli, au kupunga-pepo, shetani anajua kabisa kama angetegemea njia hiyo tu, basi angewakosa wakristo wengi sana duniani. Anafahamu kuwa mkristo mahali pake pekee anajihisi atakutana na Mungu ni kanisani na ndiko huko huko anapowafuata wakristo.

Kumbuka, shetani anatenda kazi katika SIRI, na ndiyo maana ikaitwa “SIRI YA UASI”. na inatenda kazi ndani ya Kanisa la Mungu pale shetani anapovaa mavazi ya kondoo lakini ndani ni MBWA-MWITU(Hii ni SIRI). kuharibu roho za watu(wakristo wa kweli) na kuwapeleka kuzimu. Anatumia hila zake kuwafanya watu waone kama wanamwabudu Mungu, kumbe wanamwabudu yeye.

Anaingia kanisani na kuwafanya watu wajione kuwa wapo katika njia sawa, lakini mwisho wake ni kuzimu,. Na anaowapeleka kuzimu kwa njia hii ni kubwa sana kuliko hata hizo njia nyingine ndogo ndogo kama uchawi, freemason n.k. HAPA NDIPO KRISTO ALIPOTUTILIA MSISITIZO KWAMBA “TUJIHADHARI NA MANABII WA UONGO, WANAOVAA MAVAZI YA KONDOO LAKINI NDANI NI MBWA-MWITU WAKALI”..Ndugu, Bwana hakutuonya tujihadhari na wachawi au wapiga-ramli, au freemason, au wapunga-pepo hilo ni jambo dogo sana ambalo kwa namna ya kawaida mkristo yoyote anaweza kujihadhari nayo.

Baada ya shetani kujiingiza kwa siri kwenye kanisa la Mungu na kukomaa kwa muda mrefu, tunaona alianza kwa kuharibu mafundisho ya Mungu ya kweli na kupachika mafundisho ya kipagani kama ibada za wafu, ibada za miungu mitatu, kuongeza vitabu katika NENO la Mungu, Ibada za sanamu kanisani, kubariki pombe kanisani, na kupindisha maandiko na utaratibu uliokuwepo wa kanisa kwa kupotosha ubatizo sahihi wa maji, na wa Roho Mtakatifu, kwa kuua karama za roho, kuingiza siasa na vyeo katika kanisa visivyotakana na Mungu,kuua mafundisho ya uponyaji wa kiungu,  n.k.

Kwa kuendelea hivyo alifanikiwa kutengeneza kanisa lake moja “MFU” lenye jina linalofanana na  lile kanisa la mwanzo la kweli lakini sio, watu wakidhani kuwa ndio lile kanisa la kwanza (la Mitume) kumbe wamepotea pasipo wao kujua ROHO MTAKATIFU ameshaondoka muda mrefu imebaki roho ya shetani ikitawala, Kwahiyo shetani akalipa jina hili kanisa lake akaliita UNIVERSAL CHURCH yaani KANISA LA ULIMWENGU (KANISA KATOLIKI).

Na yeye (shetani) akiwa kama mungu wa hilo kanisa aliweka watumishi wake, Na akaweka cheo cha juu zaidi kabisa katika hilo kanisa ambacho ndio cheo kile cha UPAPA (hichi ndicho cheo cha MPINGA-KRISTO mwenyewe) kisimame kwa niaba yake duniani kama Yesu Kristo alivyosimama kwa niaba ya Mungu duniani.

Tunafahamu katika historia chombo chake kiteule alichokitumia shetani kupambana na uzao wa Mungu ni KANISA KATOLIKI,na si kingine, lilifanikiwa kuua zaidi ya wakristo milioni 68, waliojaribu kuenda kinyume na mifumo yake ya kipagani. Na hadi leo kanisa hili linaendelea kuuwa watu wengi kiroho, kwa kudhani wanamwabudu Mungu kumbe wanamwabudu shetani katika hilo kanisa. Na litakuja kuuwa wengi zaidi katika kipindi cha ile dhiki kuu. HAYA NDIYO MALANGO YA KUZIMU.

Hivyo basi roho ya mpinga-kristo inakaa katika cheo cha UPAPA, kwahiyo mtu yeyote atakayekikalia hicho cheo atakuwa amekidhi vigezo vyote kuwa MPINGA-KRISTO.

Injili iliyopo leo hii, kulingana na wakati tunaoishi sio injili tu ya kuwavuta watu kwa Kristo, kwasababu wengi wameshampokea Kristo lakini hawajui kuwa wanamwabudu shetani pasipo wao kujua katika madhehebu yao wakidhani kuwa wapo sawa kumbe hawapo sawa. Ndugu Mungu kashatoa laana juu ya kanisa Katoliki na madhehebu yote yasiyokaa chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, (maana haya kwa pamoja ndiyo yanayounda ile chapa ya mnyama).  Kwa kufahamu zaidi kwa undani juu ya chapa ya mnyama unaweza kusoma soma tuliloliandika linaloitwa “CHAPA YA MNYAMA”.

Haya ndiyo maneno ya Bwana mwenyewe.

Ufunuo 18:4-5″  Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, TOKENI KWAKE, ENYI WATU WANGU, MSISHIRIKI DHAMBI ZAKE, WALA MSIPOKEE MAPIGO YAKE.

5 Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake. “

Bwana anatuonya tutoke (sio kutoka kwa miguu bali kwa roho. Yaani kujihadhari na mafundisho yote yasiotoka na Mungu, ukiri ukristo wa biblia usiukiri udhehebu) Toka katika kamba za madhehebu, umwabudu Mungu katika roho na kweli kwasababu hayo yamefanya uasherati wa kiroho kwa kuchanganya NENO la Mungu na mafundisho ya kipagani hivyo Bwana ameyahukumu na yoyote atakayeshirikiana nayo atashiriki katika mapigo yake yote yaliyoandaliwa kwasababu yameshiriki katika kumwaga damu nyingi za watakatifu wa Mungu.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

UTENDAJI KAZI WA MPINGA-KRISTO.

SIKU YA HASIRA YA BWANA

PAULO ALIMWAMBIA TIMOTHEO ATUMIE MVINYO KIDOGO KWA AJILI YA TUMBO LAKE, JE! TUNARUHUSIWA NA SISI PIA KUTUMIA POMBE?

BWANA ALIMAANISHA NINI KWENYE MSTARI HUU MARKO 2:21″ HAKUNA MTU ASHONAYE KIRAKA CHA NGUO MPYA KATIKA VAZI KUKUU;?

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2018/07/17/mpinga-kristo/