Yohana Mbatizaji anaigeuzaje mioyo ya mababa iwaelekee watoto?

by Admin | 28 August 2019 08:46 am08

Malaki 4:5 kama inasema  angalieni nitawapelekea Eliya Nabii, kabla haijaja siku ile ya BWANA, iliyo kuu na ya kuogfya. Naye ataigeuza mioyo ya Baba iwaelekee watoto wao na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.”

Kama Mungu alivyoahidi angemtua Eliya nabii. ambaye kulingana na maandiko tunafahamu Yohana mbatizaji aliyatimiza hayo maandiko kwa sehemu “A”( Yaani kuja kabla ya ile siku KUU YA BWANA) ambaye yeye alitangulia kuja kwake Kristo kwa mara ya kwanza kwa kusudi la kuigeuza Mioyo ya Baba iwaelekee Watoto.

Hii inamaanisha kwamba Yohana alihubiri injili ya kuwarejeza waalimu wa sheria na marabi wa torati pamoja na wote wanaoujia torati na kuifuatilia (ambao ndio mababa wa Torati) ili waiamini injili ya Kristo

Na tonaona…Baadhi ya wanafunzi wake mwenyewe Yohana, waliiamini Injili yake na baadaye hao hao wakaja kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo, (mfano Andrea na Yohana) ambao walikuwa hapo kwanza wanafunzi wa Yohana Mbatizaji lakini wakaja kuwa wanafunzi wa Bwana Yesu..na ndio sasa mababa wetu wa Imani ya Kikristo leo.

Hivyo Yohana mbatizaji kazi aliyoifanya ni kuwageuza Mababa wa Torati kuwa Mababa wa Imani ya Kristo.

1.Ni nani atakayeigeuza mioyo ya watoto iwaelekee mababa?

HOME

WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/08/28/yohana-mbatizaji-anaigeuzaje-mioyo-ya-mababa-iwaelekee-watoto/