by Admin | 30 August 2019 08:46 pm08
JIBU:Neno la Mungu linasema Mungu ni Roho nao wamwabuduo imewapasa wamwabudu katika roho na kweli. Wakristo hawahesabiwi haki mbele za Mungu katika siku, miezi au miaka ya kuabudia, aidha uabudu jumapili, jumatatu, jumamosi au jumatano huo ni utaratibu wa mtu tu! haimuongezei mtu chochote katika uhusiano wake na Mungu. Biblia inasema..
Wagalatia 4:9 “Bali sasa mkiisha kumjua Mungu, au zaidi kujulikana na Mungu, kwa nini kuyarejea tena mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge, yenye upungufu, ambayo mnataka kuyatumikia tena? Mnashika SIKU, NA MIEZI, NA NYAKATI NA MIAKA.”
Na Pia inasema tena katika
Wakolosai 2:16 “Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au SABATO; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.”
Hivyo Maana ya NENO sabato ni “Pumziko”, na pumziko kwa wakristo lipo rohoni, na mwokozi wetu Yesu yeye alituambia kuwa ndiye BWANA wa sabato (soma Mathayo 12:8), hivyo tukimpata YESU tumeipata SABATO au “pumziko letu la rohoni” na ndio maana anasema..
Mathayo 11:28 “ Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami NITAWAPUMZISHA. 29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; 30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.”
Kwahiyo wanaoabudu jumamosi, au jumapili au jumatano hawafanyi makosa, ni utaratibu wao tu, mbele za Mungu wote wapo sawa, kwa mfano tunasoma katika biblia wakristo wakwanza waliiteua siku ya kwanza ya juma ( yaani JUMAPILI) kwa ajili ya kukusanyika na kufanya changizo pamoja na kumega mkate,ukisoma Matendo 20:7 na 1Wakoritho 16:1-2 utaona jambo hilo, hivyo kuteua siku fulani na kusema hiyo ndio Mungu anairidhia kuabudia zaidi ya siku nyingine, ni kutokuyaelewa maandiko. kwasababu ibada halisi ipo rohoni na Mungu anaabudiwa katika roho na kweli, na sio katika siku maalumu au miezi maalumu au miaka maalumu bali ni kila saa na kila wakati mahali popote.
Ubarikiwe sana.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada zinazoendana:
BABA YANGU ANATENDA KAZI HATA SASA!.
MAMBO (2) YATAKAYOKUTENGA NA IMANI SIKU HIZI ZA MWISHO.
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/08/30/sabato-halisi-ni-lini-je-ni-jumapili-au-jumamosi-ni-siku-gani-itupasayo-kuabudu/
Copyright ©2025 unless otherwise noted.