by Admin | 31 August 2019 08:46 pm08
JIBU: Ubarikiwe dada tuisome kwanza habari yenyewe..
Marko 2: 1 “Akaingia Kapernaumu tena, baada ya siku kadha wa kadha, ikasikiwa ya kwamba yumo nyumbani.
2 Wakakusanyika watu wengi, isibaki nafasi hata mlangoni; akawa akisema nao neno lake.
3 Wakaja watu wakimletea mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanne.
4 Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza.
5 Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.
6 Na baadhi ya waandishi walikuwako huko, wameketi, wakifikiri mioyoni mwao,
7 Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu?
8 Mara Yesu akafahamu rohoni mwake kwamba wanafikiri hivyo nafsini mwao, akawaambia, Mbona mnafikiri hivi mioyoni mwenu?
9 Vyepesi ni vipi, kumwambia mwenye kupooza, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende?
10 Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (hapo amwambia yule mwenye kupooza),
11 Nakuambia, Ondoka, ujitwike godoro lako uende nyumbani kwako.
12 Mara akaondoka, akajitwika godoro lake, akatoka mbele yao wote; hata wakastaajabu wote,wakamtukuza Mungu, wakisema, Namna hii hatujapata kuiona kamwe” …
Kama ukichunguza utaona kuwa jambo la kwanza Bwana aliloliona ni ile Imani yao kwake, aliona ndani yao walikuwa na kitu cha ziada zaidi ya imani ya kuponywa, nayo ni Imani kwa Yesu Kristo…..Na tunajua kitu cha kwanza kilichomleta Bwana Yesu duniani ni kuokoa dhambi za watu, na vitu vingine baadaye…
Ukisoma Yohana 8:24 Bwana aliwaambia makutano ..“Kwa hiyo naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu”….
Unaona hapo?…Inakupasa uamini kwanza. Na ndio maana jambo la kwanza alilolitamka yeye kama mkuu wa uzima wa roho za watu mara baada ya kuona Imani yao kwake, akamwambia yule aliyekuwa amepooza..UMESAMEHEWA DHAMBI ZAKO…..Ni Neno zuri na la neema kiasi gani!!! Lakini wale wengine mawazo yao yalikuwa tofauti, wao walitazamia tu, Bwana amponye yule mtu kisha amwambie nenda zako, halafu yule mtu akaendelee kuishi maisha ya dhambi kisha mwisho wa siku afe aishie kupata hasara ya nafsi yake!..na uponyaji wake wa mwili usimfaidie kitu baada ya maisha ya hapa.
Sasa Ukiendelea kusoma pale utaona Bwana anawauliza tena wale watu, Marko 2:9 “Vyepesi ni vipi, kumwambia mwenye kupooza, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende?, Sasa kwa namna ya kawaida kwa mtu mwenye akili za rohoni atagundua kuwa ni afadhali usipone ugonjwa wako, lakini dhambi zako ziwe zimesamehewa…kuliko kuponywa halafu dhambi zako ziendeleee kubaki! Na ndio maana Bwana alimchagulia fungu lililo jema la kusamehewa dhambi zake kwanza, kisha baadaye amponye…
Na ndivyo tunavyopaswa na sisi kama wakristo kufanya sasahivi, tunakimbilia kuwaombea watu magonjwa ,wapokee miujiza, na mafanikio na huku tunasahamu kuwafundisha watu habari za msamaha wa dhambi ambao ndio msingi wa Imani ya kikristo.. vyepesi ni vipi??? Ni heri tukamuhubirie mtu habari za msamaha na toba, aokolewe roho yake hata kama hatapokea uponyaji kuliko kuhubiri kila siku mimbarani miujiza na uponyaji na huku bado watu wanakufa katika dhambi zao.
Au ni afadhali kufanya vyote kuliko kutupilia mbali habari za msamaha wa dhambi, na kushikamana na miujiza tu.
Ubarikiwe .jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/08/31/kwanini-pale-bwana-yesu-alichukua-hatua-ya-kumsamehe-dhambi-kwanza-kabla-ya-kumponya-yule-mtu-mwenye-kupoozamarko-2/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.